JEMBEKA FESTIVAL 2016, TUNAMTAKA NATURE.
Jumamosi, May 21,2016 ndiyo siku litakapopigwa Tamasha la
Jembeka Festival katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ikiwa ni Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa
Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka
Tanzania pamoja na wasanii wengine kibao.
Wakati huo huo msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini
Tanzania ambaye historia ya muziki wa Bongo Fleva hainogi bila jina lake
kutajwa, Juma Nature tayari ameangusha wino kuwa mmoja wa wasanii watakaomwaga
burudani kwenye tamasha hilo.
Jina la Sir Nature lilihusishwa mapema kabisa katika mipango
ya tamasha hilo kutokana na maombi ya mashabiki wa jiji la Mwanza na vitongoji
vyake kupitia ujumbe mfupi/ sms za vipindi tofauti tofauti ndani ya Jembe Fm
kiasi cha kuipa presha kamati husika kumuweka mkali huyo kwenye listi ya wakali
watakaopanda jukwaa moja na Neyo.
Licha ya msanii huyo kufanya makamuzi jijini Mwanza mapema
mwezi Machi akipanda jukwaa moja na wakali wengine kutoka nchini Nigeria Tekno,
Seyi Shey na Ommy Dimpoz kutoka nchini Tanzania nyota yake imeonekana kung'ara
tena katika kuelekea JEMBEKA NA VODACOM.
"Haijalishi mara
ngapi ndani ya mwaka huu Nature kaja Mwanza na tukaenda kwenye show zake.
Tunamtaka Nature" Anasema mmoja wa mashabiki wa burudani Jijini Mwanza.
List ya wasanii wengine watakao husishwa na tamasha hilo
mpaka sasa bado haijatajwa rasmi, licha ya fununu kwa baadhi ya wakali. Kumbuka
ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi
10,000, 50,000 na 100,000 so anza kujichanga mapema mwana wa kwetu.
Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako.
Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK
Security, JembeFm- JembeniJembe, Gsengo Blog, Michuzi Blog, Binagi Blog na
wadau wengine.
Nunua Tiketi yako mapema www.jembenijembe.com
Bonyeza HAPA Kujua Utamu wa Jembeka 2016
No comments: