LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAZAMA SHAMRASHAMRA ZA USHINDI WA MABULA JIJINI MWANZA, BAADA YA MAHAKAMA KUFUTA KESI DHIDI YAKE.

Mapema leo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (mwenye tai) kutoka CCM akiwa katika Ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza akisubiri kusomwa kwa maamuzi ya Kesi ya Kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyofunguliwa na aliekuwa mbunge na mgombea wa Chadema Ezekiel Wenje.

Jaji wa Mahakama hiyo Kakusulo Sambo, ametupilia mbali kesi hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kutokana na kukosa ushahidi wa kuthibitisha kuwa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa katika vituo 27 kati ya Vituo 666 Jimboni Nyamagana yalikuwa na figisu figisu. 

Wenje hakuwepo Mahakamani na katika taarifa yake kwenye mahojiano na Radio Saut ya Jijini Mwanza, amesema atakata rufaa dhidi ya maamuzi yaliyotolewa hii leo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mapema leo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (mwenye tai) akifurahia ushindi na Wakili wake Constantin Mtalemwa.
Mapema leo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (Katikati) akitoka nje akiwa pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia).
Viongozi wa CCM Mkoani Mwanza pamoja na Wafuasi wa chama hicho wakifurahia ushindi wa Mabula Mahakamani katikati ya Jiji la Mwanza kuelekea Ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (katikati) akisalimiana na wana CCM katika ofisi za Chama Mkoa wa Mwanza baada ya Ushindi. Amesema ushindi wa Mabula Octoba 25 mwaka jana na wa hii leo mahakamani umefungua milango mipya ya Mabula kuwatumikia wananchi. Amesema chama kitazungumza na Mawakili wa Mabula ili kupata gharama zilizotumika katika kesi hiyo ili zilipwe na Wenje kama Maamuzi ya Mahakama kufuta shauri la Wenje kwa gharama lilivyotolewa hii leo.
Shangwe za Wana CCM katika ofisi za chama Mkoa wa Mwanza
Wafuasi wa CCM wakimsindikiza Mabula kutoka katika ofisi za Chama Mkoa, kwenda katika Ofisi za Chama Wilaya ya Nyamagana
Wana CCM wakifurahia ushindi wa Mabula Mahakamani nje ya Ofisi za Chama Wilaya ya Nyamagana
Wana CCM wakikumbushia enzi za Kampeni
Kutoka Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Elias Mpanda, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) wakiwa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana baada ya ushindi dhidi ya kesi iliyokuwa imefunguliwa na Wenje.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula akizungumza na Wanahabari baada ya Ushindi dhidi ya Kesi iliyokuwa ikimkabiri.
Hali ya Ulinzi ilikuwa imeimarishwa Jijini Mwanza
Shamra shamra zilipambwa na mabango mbalimbali Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kujikumbushia Ushindi wa Mabula

No comments:

Powered by Blogger.