LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFANYAKAZI WA UJENZI WA JENGO LA HOTEL YA NYOTA TANO JIJI MWANZA WAGOMA.

Wafanyakazi wa ujenzi wa jengo la hotel yenye hadhi ya nyota tano katika eneo la Capripoint Jijini Mwanza, wamegoma kufanya kazi ili kushinikiza stahiki zao.

Wakizungumza kufuatia mgomo huo, Wafanyakazi hao kutoka Kampuni ya ujenzi ya China Railway Jianchang CRJ ya kutoka nchini nchina, wamesema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na mwajiri wao tangu mwaka 2013 na kwamba wamekuwa wakitukanwa matusi ya udharirishaji, mbali na kunyanyaswa katika mafao yao pamoja na vitendea kazi.

Kufuatia hali, wameomba viongozi wanaohusika Mkoani Mwanza, kuhakikisha kwamba madai yao yanatatuliwa huku wakimuomba rais John Pombe Magufuli kuingilia kati ili kusaidia kupata stahiki zao.

Uongozi wa Kampuni hiyo haukuweza kupatikana ili kuzungumzia mgomo huo, ambapo juhudi za kuutafuta bado zinaendelea.

Kampuni ya ujenzi ya CRJ inajenga jengo refu kuliko yote Jijini Mwanza, likiwa na ghorofa 15 ambapo jengo hilo ni mali ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii la NSSF ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 72.

No comments:

Powered by Blogger.