LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAJAMBAZI KAHAMA MKOANI SHINYANGA YAACHA MAJONZI.

Na:Shaban Njia
Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga juzi uliingia katika majonzi mazito huku ukisimamisha shughuli zake kwa muda wa masaa matatu baada ya majambazi waliokuwa wakitaka kufanya jaribio la kuvamia duka la mfanyabiashara mmoja mjini humo kutupiana risasi na polisi.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 za jioni katika eneo la katikati ya mji wa Kahama ambapo majambazi hayo yalivamia katika duka la mfanyabiashara Emanuel Mkumbo kwa lengo la kupora fedha.

Hata hivyo majambazi hayo hayo baada ya kuvamia kwa mfanyabiashara huyo na kukosa fedha yaliamua kumpiga risasi na kumua na kisha kuanza kukimbia kabla ya jeshi la polisi kuingilia kati na kisha kuanza kurushiana risasi.

Jeshi la Polisi Wilayani Kahama lilifanikiwa kuwauwa majambazi matatu, huku pia majambazi hayo yakiwauwa kwa kuwapiga risasi raia wawili ambao ni mmiliki wa duka lililovamiwa pamoja na dereva mmoja wa lori ambae jina lake halikufahamika mara moja.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, SPC Dismas Kisusi, alisema kuwa katika tukio hilo jeshi la Polisi Wilayani Kahama lilifanikiwa kuwapora majambazi hao bunduki mbili za kivita moja aina ya UZGUN na nyingine SMG, kisu kimoja cha kijeshi pamoja na bomu moja  la kutupa kwa mkono.

No comments:

Powered by Blogger.