LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAJIVUNIA UWAKILISHI WA MTOTO GETRUDE CLEMENT KATIKA MKUTANO WA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA.

Watanzania wamefurahishwa na uwakilishi wa Mwanahabari Mtoto Getrude Clement (16) kutoka Mtandao wa Wanahabari Watoto Mkoani Mwanza aliliwakilisha vyema Taifa, baada ya kuhutubia kwa kujiamini katika Mkutano wa Baraza Umoja wa Mataifa uliofanyika Jijini New York nchini Marekani.

Katika Mitandao ya Kijamii, Watanzania wametoa pongezi nyingi kwa Getrude ambapo mwanahabari Simba Kabonga amesema "Getruda ni hazina ya nchi, hadi sasa", huku wengine wakisifu hotuba iliyotolewa na mtoto huyo.

Mkutano ambao ulihusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, ulihudhuriwa na Marais 60 kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo Mataifa 15o yalisaidi mkataba wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi hususani kuzuia uchafuzi wa mazingira.  

Ulipowadia wasaa wa kuongea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bank Moon alimkaribisha Getrude ambae aliongea kwa kujiamini kama anavyoonekana katika Video hapo chini.

#MwanzaInajivuaWewe #TanzaniaInajivuniaWewe #AfrikaInajivuniaWewe #DuniaInajivuniaWewe #TutambueVipajiVyaWatotoNaKuviendeleza.
Binagi Blog-BMG tunatoa pongezi za dhati kwa shujaa Getrude kwa kuwawakilisha vyema watoto, Vijana pamoja na Watanzania kwa ujumla.

No comments:

Powered by Blogger.