BASI LA MWENDO KASI DAR LAUA.
Baadhi ya wananchi wakiweka mwili wa mtoto,
Nasra Mkinze, mwanafunzi wa darasa la pili, baada ya kugongwa na basi la mwendo kasi akiwa amebebwa kwenye pikipiki leo mchana jijini Dar ambapo haikufahamika mara moja jina
la shule aliyokuwa akisoma.
Ni baada ya basi la mwendo kasi lenye nambari T.953 DGV kuigonga pikipiki (bodaboda) yenye nambari MC 351 AWX ambapo dereva wa bodaboda alitaka kuwahi kupita katika mataa Shekilango.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari kwenda kuhifadhiwa
Bado utii wa sheria za usalama barabarani hususani katika barabara za mabasi yaendayo kasi Jijini Dar es salaam hauzingatiwi hivyo BMG tunashauri wananchi, abiria na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia utii matumizi sahihi ya barabara ili kuepukana na ajali zisizo za lazima.
Picha na Khamis Mussa
No comments: