LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADIWANI KASULU VIJIJINI MKOANI KIGOMA WANG'AKA KWA UPOTEVU WA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI TANO.


Na Rhoda Ezekiel, Kigoma.
Baraza la Madiwani  katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Vijijini Mkoani Kigoma, limemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anawafuatilia watendaji  waliosababisha upotevu wa zaidi ya shilingi Bilioni tano zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi wa maendeleo ya miradi ya Wananchi.

Wakizungumza katika Baraza hilo jana, baadhi ya madiwani walimuomba Mkurugenzi kufanya uchunguzi  wa upotevu wa fedha hizo na majibu yatolewe hadharani ili fedha hizo zirudishwe na ziweze kufanya kazi iliyo kusudiwa na suala hilo kukumbushwa katika kila baraza litakalofanyika.

Diwani wa Kata ya Makere, Poteza Kikali alisema fedha hizo zimepotea muda mrefu tangu baraza lililopita waliomba fedha hizo zirudishwe lakini mpakasasa imeundwa tume ya uchunguzi iliyotumwa na katibu tawara wa Mkoa kufuatilia suala hilo lakini bado hatuja patiwa majibu tunaomba ikiwezekana lifikishwe ngazi za juu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kasulu vijijini, mhe Vuma Holle alisema fedha hizo ni nyingi sana na kunamiradi mingi imeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na upotevu wa fedha hizo tunamuomba Mkurugenzi afuatilie ziweze kurudishwa zifanye kazi zilizokusudiwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu  vijijini, Paulo Malala,  alisema  suala la upotevu wa fedha hizo lipo kwa Katibu tawala wa Mkoa linaendelea na uchunguzi likikamilika litaletwa mbele ya madiwani lijadiliwe na fedha zirudishwe kwenye miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kasulu vijijini, Saidi Ndiyunze, aliwaomba madiwani kuendelea kuviamini vyombo vya dola na kuviacha vifanye kazi  bila kuviingilia  kwani bado kuna mambo uchunguzi unaendelea hivyo madiwani wa baraza hilo wawe wavumilivu.

No comments:

Powered by Blogger.