LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC KAHAMA AIBANA KAMPUNI YA ACACIA.


Na Shaban Njia
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, Vita Kawawa, amewataka wawekezaji wa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani humo, kuhakikisha inatoa taarifa zilizo sahihi za makampuni yanayotakiwa kulipa ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Mji wa Kahama.

Kawawa aliyasema hayo majuzi katika hafla ya kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni  588 ziliztolewa na mgodi huo kama ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Mji wa Kahama katika kipindi cha kuanzia mwezi julai  hadi mwezi disemba mwaka jana.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Asa Mwaipopo, akikabidhi hundi hiyo kwa Mkuu huyo wa Wilaya, alisema ulipwaji wakodi unatokana na mafanikio yaliopatikana katika kipindi hicho cha miezi sita iliyopita na kuwataka wananchi kuendelea kuuamini mgodi na kutoa ushirikiano pale panapohitajika.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Abel Shija, alisema kuwa fedha hizo lazima ziwafikie wananchi kwa wakati na kuongeza fedha hizo zitatumika vyema kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa.

No comments:

Powered by Blogger.