LIVE STREAM ADS

Header Ads

DUKA LA "GET WELL MEDICS" LA JIJINI MWANZA MATATANI.


Judith Ferdinand, Mwanza
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Ofisi ya Kanda ya Ziwa, imelifunga duka la kuuza dawa za binadamu la "Get Well Medics" kwa kukutwa likitengeneza vinywaji aina ya juisi kinyume na sheria.

Mkaguzi wa Chakula wa TFDA Kanda ya Ziwa, Makaya Nsonda, amesema, wameamua kulifunga duka hilo lililoko eneo la Igoma jijini la Mwanza, kutokana na kukutwa  likizalisha juisi kinyume na Sheria.

Amesema bidhaa  zilizokutwa katika duka hilo ni juisi aina ya Poa Fruit Drink ambapo kulikuwa na chupa 470 zikiwa zimekwisha fungashwa tayari kwa kuingia sokoni huku chupa 300  zikiwa hazijawekwa vinywaji.

Pia Nsonda alieleza kuwa, ndani ya duka hilo  walikuta muhuri uliokuwa ukitumika kuweka tarehe ya mwisho ya matumizi ya bidhaa pamoja na vyombo kama vile diaba na chujio  vinavyosadikiwa kutumika kutengenezea bidhaa hizo.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa TFDA pale wanapokutana na bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ambazo wanazitilia mashaka, kwani suala la udhibiti wa bidhaa hizo ni jukumu la jamii nzima.

No comments:

Powered by Blogger.