LIVE STREAM ADS

Header Ads

INASIKITISHA, MAUAJI MENGINE YAFANYIKA MKOANI MWANZA.

Inasikitisha. Maisha ya watu sasa yako Mikononi mwa baadhi ya watu. Kuishi au Kufa ni maamuzi ya wahalifu wachache. Siku chache zilizopita, watu saba wa familia moja waliuawa kwa kukatwa mapanga katika Kijiji cha Nyigumba, Kata ya Sima Wilayani Sengerema. Yakafuatia mauaji ya waumini watatu akiwemo imamu wa msikiti, waliokuwa wakiswali katika msikiti wa Rahman katika Kata ya Mkolani Jijini Mwanza.
Jana saa moja jioni Jijini Mwanza, Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Bulale Kata ya Buhongwa, Alphonce Mussa, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu ambao bado hawajajulikana ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kikao na wajumbe wa serikali ya mtaa.
MAUAJI YA KIHOLELA YANAYOENDELEA MKOANI MWANZA, YATAZAMWE KWA JICHO LA PILI KWANI YANAWEZA KUATHIRI SHUGHULI NYINGI IKIWEMO ZA KIUWEKEZAJI.

No comments:

Powered by Blogger.