LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAMASHA LA KUSAKA VIPAJI VYA UTANGAZAJI LA "HHC ALIVE TALENT SEARCH" JIJINI MWANZA LAIBUA VIPAJI VIPYA.

Kushoto ni Meneja wa kituo cha Radio cha 91.9 HHC ALIVE cha Jijini Mwanza, Maganga James Gwensaga, akizungumza katika tamasha la kusaka Vipaji vya Utangazaji (HHC ALIVE TALENT SEARCH 2016) lilizofanyika katika Kanisa la HHC Cathedral, Ilemela Mkoani Mwanza.

Watangazaji chipukizi, Hellen Jerome, Ibrahim Mgaya pamoja na Deophinius Salvatory, wameibuka kidedea katika tamasha la kusaka Vipaji vya Utangazaji lililoandaliwa na kituo cha redio cha 91.9 HHC Alive cha Jijini Mwanza.

Tamasha hilo ambalo lilifanyika juzi jumamosi ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika, liliwashirikisha washiriki zaidi ya 50 ambao walichujwa na kubakia 22 walioingia katika fainali, ambapo kati ya hao washiriki watatu walioonyesha uwezo wa kutangaza, wamejiunga na radio hiyo kwa ajili ya kufuliwa zaidi ili kuwa watangazaji mahiri.

Mratibu wa tamasha hilo, Papaa Jose alisema lengo la tamasha hilo ni kuibua vipaji vya utangazaji vilivyolala ambavyo anaamini kwamba vikiibuliwa vitaleta mapinduzi katika tasnia ya utangazaji.

Meneja wa HHC Alive, Maganga James Gwensaga, alisema tamasha hilo ni mwanzo wa matamasha mengine yanayotarajiwa kuratibiwa na redio hiyo ili kuibua vipaji zaidi ambavyo hupotea kwa kutoibuliwa.

Washiriki wa tamasha hilo, walipongeza uthubutu uliofanywa na redio ya HHC Alive katika kuibua na kuajiri vijana wenye vipaji ambavyo vinapotea mitaani ambapo waliomba tamasha hilo kufanyika kila mwaka.

Mkurugenzi wa HHC Alive, Askofu Eugen Mulisa, aliwapongeza washiriki wote na kuwahimiza kuongeza juhudi zaidi ili kufikia ndoto zao na kwamba vipawa walivyonavyo vinaweza kubadilisha maisha yao kwa kusonga mbele zaidi kimaendeleo.
Washiriki wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji jijini Mwanza, waliongia hatua ya sita bora.
Washindi wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji lililoratibiwa na kituo cha redio cha HHC Alive cha Jijini Mwanza. Kushoto ni Ibrahim Mgaya, katikati ni Hellen Jerome na kulia ni Deophinius Salvatory.
Washiriki wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji jijini Mwanza, wakiwa katika picha ya pamoja na majaji pamoja na baadhi ya watangazaji wa HHC Alive Fm.
Washiriki wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji, wakionyesha uwezo wao wa kutangaza.
Miongoni mwa washiriki wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji, wakionyesha uwezo wao wa kutangaza.
Mmoja wa washiriki wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji, wakionyesha uwezo wao wa kutangaza.
Majaji wakiendelea kufuatilia vipaji, ambapo kutoka kushoto ni Maganga James Gwensaga (Meneja HHC Alive), Neema Charles (Mkombozi Fm) na George Binagi-GB Pazzo (102.5 Lake Fm & Binagi Blog).
Majaji wakitafuta jina la kukata. Zoezi liliendeshwa kwa uwazi wa hali ya juu
Mkurugenzi wa HHC Alive, Askofu Eugen Mulisa, akifungua tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji jijini Mwanza.
Washiriki wa tamasha la kusaka vipaji vya utangazi, lililoandaliwa na redio HHC Alive ya Jijini Mwanza
Baadhi ya watangazaji wa HHC ALIVE
Kulia ni mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Vanessa Laban akitumbuiza katika tamasha la kusaka vipaji vya utangazaji jijini Mwanza. Kushoto ni mmoja wa washiriki wa tamasha hilo alieguswa na uimbaji wa Vanessa akicheza nae jukwaani.
Kwaya ya Kanisa la HHC Cathedral ikitumbuiza katika tamasha hilo.
Meneja wa HHC Alive Fm, Maganga James Gwensaga (Kushoto) akiwa pamoja na Mussa BMG.
Picha na Mussa BMG.

No comments:

Powered by Blogger.