LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA MKOA WA SHINYANGA WAFANA.



Hapa ni katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala, kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo jana jumapili Mei 22,2016 Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga (Ahmadiyya Muslim Jamaat Shinyanga) ilifanya mkutano wa mwaka wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga ukiwa na kauli mbiu ya " Love For All Hatred For None (Mapenzi Kwa Wote Bila Chuki Kwa Yeyote".
Mgeni rasmi alikuwa katibu tawala msaidizi idara ya  uchumi na uzalishaji aliyemwakilisha kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella huku waumini wa dini hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakihudhuria mkutano huo.

Mkutano huo uliolenga kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu hali itakayosaidia kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na albino, umehudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (pichani juu).

Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alieleza kusikitishwa na kitendo cha mauaji ya watu watu msikitini na kuongeza kuwa dini ya kiislam hairuhusu vitendo kama hivyo huku akiviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika wa kitendo hicho haramu.

Kupitia mkutano huo jamii imeelimishwa juu ya dhana potofu dhidi ya uislamu ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha dini hiyo pamoja na vikundi vya kigaidi mfano wa Boko haram, Isis, Al-shabaab na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikidhuru binadamu. 

Mada mbalimbali zimetolewa na viongozi wa jumuiya hiyo ikiwemo nafasi ya dini katika maisha ya binadamu, malezi ya watoto na majukumu ya wazazi sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu, umuhimu wa kuwa kiongozi (Khalifa) wa kiroho na barakaza ukhalifa pamoja na masharti ya kujiunga na jumuiya hiyo(masharti 10 ya Baiat na wajibu wa waumini.
Hapa ndipo Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga waumini wa dini ya kiislamu kutoka Jumuiya hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kwa wingi kusikiliza mawaidha mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Jumuiya hiyo pamoja na wageni waalikwa akiwemo kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Idd Nchira
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitoa mada kuhusu Haja ya nafasi ya dini katika maisha ya binadamu ambapo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kutenda mambo mema na kujiepusha na vitendo vya kihalifu ikiwemo kuua watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

Alisisitiza kuwa uislamu ni dini ya amani hivyo kuwataka binadamu kuishi kwa amani na kwamba kitendo cha kuua mtu mmoja ni sawa na kuua dunia nzima.Hata Hivyo Ame alisema sera ya jumuiya hiyo ni kutochanganya siasa na dini 
Meza kuu,wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry,kushoto kwake ni mgeni rasmi Mohammed Idd Nchira,akifuatiwa na rais wa Jumuiya hiyo Kanda ya Ziwa Salim Thani,wa kwanza kushoto ni Naibu rais wa jumuiya hiyo Kanda ya ziwa Yahaya Kamba Ulaya.Wa kwanza kulia ni Mbashiri wa kanda ya ziwa  wa jumuiya hiyo Sheikh Waseem Khan 
Waumini wa dini ya Kiislam kutoka maeneo ya mjini na Vijijini ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga waliojitokeza katika mkutano huo
Mgeni rasmi katika mkutano huo Mohammed Idd Nchira akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ambapo alisema suala amani katika jamii ni watu wote hivyo kuwataka watanzania kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kutenda uhalifu
Aliyesimama ni Afisa wa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upepelezi na makosa ya jinai mkoa wa Shinyanga Issa Ramadhan akitoa neno ambapo alisema jamii yenye malezi mema haiwezi kuwa na vitendo vya kihalifu na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua watu wote wanaofanya vitendo vya uhalifu.
Wanawake wa Kiislam wakiwa katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa mwaka,ambapo kwa mara ya pili sasa mkutano kama huo unafanyika mkoani Shinyanga, mkutano mwingine ulifanyika mwaka 2014.
Wanawake wakiwa msikitini
Mkuu wa kituo cha polisi Tinde Mkaguzi Msaidizi wa polisi Wilbert Sichone aliyemwakilisha mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga,akitoa neno katika mkutano huo ambapo aliwaomba viongozi wa dini mbalimbali kuendelea kutoa elimu ya dini kwani vitendo vingi vya kihalifu vimekuwa vikijitokeza kutokana na jamii kutokuwa na hofu
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsalala kilichopo katika kata ya Tinde Sandeko Machongo akitoa shukrani kwa jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wananchiwa kijiji hicho katika masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa visima vitatu vya maji
Waumini wakifutilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano huo
Mbashiri/Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Morogoro Asif Butt akitoa mada ya Masharti kumi ya Baiat na wajibu wa waumini wa jumuiya hiyo.Miongoni mwa masharti hayo ni pamojana waumini kutojihusha na vitendo vya kishirikina akieleza kuwa ushirikina ndiyo chachu ya maovu/mabaya yote katika jamii
Mbashiri wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Morogoro Asif Butt alitumia fursa hiyo kuwataka wanadamu kuwapuuza baadhi ya watu wanaodai kuwa jumuiya hiyo haifuati misingi ya dini ya kiislam huku akiongeza kuwa tofauti yao na wengine wao wanafanya misingi ya dini kwa vitendo badala ya maneno
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo
Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akitoa hotuba yake ambapo pamoja na mambo mengine alisema jumuiya hiyo ambayo ipo katika nchi 207 duniani kila siku imekuwa ikiwakumbusha waumini kuishi katika misingi ya kumfuata mwenyezi mungu,kwasisitiza waumini kushika mafundisho kwa vitendo badala ya maneno ili wawe raia wema ili jamii iishi kwa amani
Kulia ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitafsiri hotuba ya Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry aliyokuwa anaitoa kwa lugha ya Kiingereza.
Imeandaliwa na Kadama Malunde

No comments:

Powered by Blogger.