LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WASHUHUDIA BURUDANI KALI KATIKA TAMASHA LA JEMBEKA.

Jumamosi Mei 21 kuamkia Jumapili Mei 22, imekuwa full shangwe jijini Mwanza katika Tamasha la "Jembeka Festival 2016", baada ya kudondoshwa burudani kali kutoka kwa msanii Neyo (Marekani) pamoja na wasanii wengine nchini wakiongozwa na Diamond Platnumz, katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Ni tamasha ambalo hufanyika kila mwaka mei 21, kama sehemu ya maadhimisho ya ujio wa jembe fm radio ya jijini Mwanza.

Diamond Platnumz akizungumza na Vesterjtz #BMG baada ya show, ambapo amesisitiza wasanii kufanya kazi kwa bidiii na kwa ubunifu ili kufikia level aliyofikia. Pia amewasihi watanzania kuendelea kumpigia kura ili aweze kunyakua tuzo ya BET 2016 alizotajwa kushiriki.
Msanii Fid Q akizungumza na wanahabari baada ya show ambapo amepongeza namna tamasha la Jembeka 2016 lilivyofana.
Diamond Platnumz akiperfom katika tamasha la Jembeka 2016
Msanii Neyo kutoka nchini Marekani akitoa burudani katika tamasha la Jembeka Jijini Mwanza
Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza walifurika katika tamasha la Jembeka huku pia likihudhuriwa na wapenzi wa burudani kutoka mikoani
Maelfu ya wananchi wakifuatilia burudani katika tamasha la Jembeka 2016
Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza walifurika katika tamasha la Jembeka huku pia likihudhuriwa na wapenzi wa burudani kutoka mikoani
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula akizungumza na BMG katika tamasha la Jembeka ambapo alipongeza namna tamasha hilo lilivyofana na kutanabaisha kwamba ni tamasha bora Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Moses Nhauye, ambae alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la Jembeka 2016, akizungumza na wanahabari ambapo alieza kufurahishwa na namna jiji la mwanza linavyokuwa na hivyo kuvutia matamasha makubwa kufanyika tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kuwa matamasha hayo hufanyika Dar es salaam pekee.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, akizungumza na BMG katika tamasha la Jembeka ambapo amesisitiza vijana wenye vipaji kusaidiwa ili waweze kufikia mafanikio yao ikizingatiwa kwamba muziki sasa ni ajira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira, Mhe.January Makamba, akizungumza na BMG katika tamasha la Jembeka, ambapo alisema tamasha hilo litatoa hamasa kwa wasanii wa Mwanza kuongeza juhudi katika muziki ili kufikia mafanikio yao.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza na BMG katika tamasha la Jembeka 2016 ambapo alipongeza mafanikio ya tamasha hilo huku akiwakaribisha wawekezaji wengine kuwekeza Mwanza kwa kuwa ni Mkoa wenye fursa za uwekezaji.
Kulia ni Msanii Mr.Blue akizungumza na VesterJtz katika tamasha la Jembeka 2016
Msanii G-rick kutoka Jijini Mwanza amefurahia namna tamasha hilo linavyotoa fursa katika kuukuza muziki wa Mwanza.
Kulia ni Msanii Elizayo HB, akizungumza na BMG katika tamasha la Jembeka 2016 ambapo alisema tamasha hilo ambalo limewaleta Neyo na Diamond Mwanza, limemjenga maraduru lengo likiwa ni kuhakikisha anafikia mafanikio kama ya wasanii hao.
Shabiki wa burudani jijini Mwanza, akizungumza na BMG ambapo amepongeza namna wasanii mbalimbali akiwemo Diamond walivyodondosha burudani poa.
Mtangazaji wa Citizen Radio Kenya, D-Mike Presenter (Kushoto) akizungumzia tamasha la Jembeka ambapo amesema kuwa limekuwa ni tamasha la kufana sana.
George Binagi-GB Pazzo, Mhe.Makamba na VesterJtz
Imeandaliwa na BMG

No comments:

Powered by Blogger.