LIVE STREAM ADS

Header Ads

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO MAALUMU KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kufikia tamati kesho Mei 07,2016.
Na:BMG

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba, amewataka watumishi wa Mahakama Mkoani Mwanza kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Mhe.Makaramba ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.

Amesema Mafunzo hayo yamekuja kwa wakati ikizingatiwa kwamba Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya Utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kwamba inatoa huduma iliyo bora kwa wananchi.

Mwenyekiti wa taasisi ya MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa katika Kanda zote za Mahakama nchini, baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2014 kuonyesha kwamba kuna ugumu katika upatikanaji wa habari za mahakama kwa umma hata kama habari hizo siyo za siri.

“Tunaipongeza Mahakama kwa hatua hii ya kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wake na kutoa taarifa muhimu kwa wananchi maana mihimili mingine imekuwa ikiminya upatikanaji wa taarifa zake hata kama taarifa hizo siyo za siri”. Amesema Berege.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza ujuzi zaidi wa namna ya kuwahudumia wateja (Wananchi) ili kuwafanya watambue kwamba Mahakama nchini zinatenda haki.

Mafunzo hayo ambayo yanafadhiriwa na Shirika la Misaada la Ujerumani FES, yamefanyika Mkoani Mwanza baada ya mafunzo kama hayo yaliyofanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tabora kuonyesha yameongeza ufanisi na utendaji wa Watumishi wa Mahakama katika kuwahudumia wananchi hususani katika utoaji wa taarifa kwa umma ambapo yanawajumuisha Mahakimu, Watunza Kumbukumbu, pamoja na Maafisa Utumishi wa Mahakama.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza, wakimsikiliza Mhe.Robert Vicent Makaramba mabae ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza. 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege, akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege, akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege (Kulia), akifurahia jambo wakati wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Wakili na Mwanahabari James Marenga 
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza katika Mafunzo hayo
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza katika Mafunzo hayo
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza, wakifurahia hotuba ya mgeni rasmi, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Mgeni Rasmi, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramamba (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Mgeni Rasmi, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramamba (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.