LIVE STREAM ADS

Header Ads

JAJI MKUU KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI 2016 MWANZA.

Mwenyekitiki wa MisaTan, Simon Berege (katikati) akitoa taarifa kwa wanahabari juu ya Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2016.

Getruda Ntakije na Judithi Ferdinand, Mwanza
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka huu, yanayotarajia kufanyikia kitaifa Mkoani Mwanza Mei mbili na tatu.

Wageni wengine wanaotarajiwa kushiriki katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer pamoja na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues.

Akitoa taarifa kwa wanahabari juu ya maadhimisho hayo hii leo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania MISA Tanzania, Simon Berege, amesema maadhimisho hayo hutumika kama jukwaa ambalo hutumiwa na wadau wa vyombo vya habari kushinikiza mataifa mbalimbali duniani kutengeneza sheria rafiki za vyombo vya habari zinazoweza kuhakikisha uhuru wa habari katika nchi zao unafuatwa.

Alisema, maadhimisho ya mwaka huu yanaadhimishwa pamoja na matukio matatu ya kihistoria ambayo ni maadhimisho ya miaka 250 ya sheria ya kwanza ya uhuru wa habari duniani, miaka 25 ya kupitishwa kwa Azimio la Windhoek ambalo ni azimio la kanuni ya uhuru wa habari na 2016 ambao ni mwaka wa kwanza wa mazungumzo wa miaka 15 wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Vyombo vya Habari.

"Siku hii hutumika kama jukwaa ambalo hutumiwa na wadau wa vyombo vya habari kushinikiza mataifa kutengeneza sheria rafiki za vyombo vya habari zinazoweza kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari katika nchi zao".Amesema Berege.

Amesema kutokana na hali hiyo, maadhimisho hayo mwaka huu yanaonyesha uhusiano kati ya uhuru wa habari, utamaduni wa uwazi na haki ya uhuru wa habari, na maendeleo endelevu katika wakati wa digital ambapo jambo la msingi katika hayo ni jukumu la msingi kwa waandishi wa habari pamoja na umuhimu wa kuwalinda wale ambao huleta huduma hiyo kwa jamii ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Kupata taarifa ni haki yako ya msingi, Idai".

Afisa Habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UN), Usia Ledama, amesema umoja huo unathamini mchango wa vyombo vya habari katika jamii hivyo wanaungana katika maadhimisho hayo na kwamba wanamini bila kuwa na uhuru wa vyombo vya Habari mataifa hayawezi kuendelea.
Bonyeza HAPA Kutazama Video

No comments:

Powered by Blogger.