LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA JUU YA HALI YA VYOMBO VYA HABARI KUZINDULIWA JIJINI MWANZA.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania, MISA TANZANIA, Simon Berege (katikati) akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016, yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Mkoani Mwanza kuanzia kesho Mei 2 na 3 katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Na:George Binagi

"Taarifa kuhusu hali ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA, ijulikanayo kama JE HII NI HAKI? itazinduliwa sambamba na Sera ya Jinsia Kwa Vyombo vya Habari vya Jamii". Amesema Berege.

Aidha ameongeza kuwa pia kutakuwa na mijadala juu ya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Upatikanaji wa Habari pamoja na Muswada wa Huduma ya Habari.

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, huku viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nhauye.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania, MISA TANZANIA, Simon Berege (katikati) akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016, yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Mkoani Mwanza kuanzia kesho Mei 2 na 3 katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Jane Mihanji (Kulia), akizungumzia Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Dunia 2016, yanayofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza. Amesisitiza wanahabari kutimiza wajibuo wao wa kuihabarisha jamii.
Raziah Mwawanga (Kulia) kutoka Wakfu wa Vyombo vya Habari (Tanzania Media Foundatio) akizingumzia Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016.
Amewasihi wanahabari kuitumia Siku hiyo kuthamini na kukumbuka walikotoka katika kupigania uhuru wa vyombo vya habari.
Neville Meena ambae ni Katibu wa Baraza la Wahariri Tanzania (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka huu. 
Amewahimiza Wanahabari kuitumia siku hiyo kwa ajili ya kutafakari juu ya haki zao badala ya kuwa watetezi wa watu wengine huku wao wakibaki nyumba katika utetezi wa haki zao.
Usia Nkoma ambae ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO nchini Tanzania.
Wanahabari na Wadau wa Habari.
Wanahabari. 
Shukurani za pekee ziwaendee Misa-Tanzania, UNESCO, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja wa Mataifa Ofisi ya Tanzania, Taasisi ya Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania (KAS), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Klabu ya Waandishi wa Habari Mwanza (UTPC) Pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuhakikisha Maadhimisho hayo yanafanikiwa.

No comments:

Powered by Blogger.