LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WATAKIWA KUFANYA KAZI KUENDANA NA KASI YA DKT.MAGUFULI.

Na:Judith Ndibalema
Wafanyakazi na Watendaji wa sekta mbalimbali Mkoani Mwanza, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na  uadilifu, ili kuendana na kasi ya rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Jonh Mongella, ambaye alikua mgeni rasmi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi), ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Misungwi.

Alisema, wafanyakazi kazi wengi wanakabiliwa na tatizo la kutofanya kazi kwa bidii na uadilifu.

Pia alisema, lengo la awamu ya tano ni kila mfanyakazi kutimiza wajibu, ili kuleta ufanisi wa kazi na kuchochea maendeleo ya taifa kwani ukifanya uzembe utatumbuliwa.

'' Ukileta urembo na kujifanya mkubwa  utatumbuliwa na kurudi kijijini, kwani serikali ya awamu ya tano inaitaji kila mfanyakazi kutimiza wajibu katika nafasi yake, ili kuleta ufanisi," alisema Mongella.

Naye Katibu wa Shirikisho la Vyama Uhuru vya Wafanyakazi  Tanzania (TUCTA) mkoa wa Mwanza, Zebedayo Athuman  aliiomba serikali kuboresha reli ya kati, ili kupunguza gharama za bidhaa na usafirishaji sambamba na kupunguza bei za mafuta  na gesi,hali itakayosaidia wafanyakazi na wananchi kumudu.

Pia aliiomba serikali kuwainu kiuchumi wafanyakazi kama kaulimbiu ya maadhimisho hayo inavyosema " Dhana ya mabadiliko ilenge kuinua hali za wafanyakazi ".

Kwa upande wake Ofisa Elimu, Vifaa na Takwimu Idara ya Elimu Sekondari Misungwi Nyandaro Msagaswa alisema, ni wakati wa wafanyakazi kutimiza wajibu kulingana na mipango kazi waliojiwekea ikiwa ni pamoja na kujituma na kuwa tayari wakati wote.

Pia alisema kiwango cha mshahara siyo kibaya ila makato ya kodi ni makubwa inapelekea kutokidhi mahitaji yao, hivyo aliiomba serikali kupunguza kodi kwenye mishahara hayo.

No comments:

Powered by Blogger.