LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAFULILA KUJIPANGA UPYA BAADA YA KUSHINDWA KESI YA UCHAGUZI.

Na Rhoda  Ezekiel, Kigoma
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, imetupilia mbali maombi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, David Kafulila, ya kupinga  matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, Hasna Mwillima (CCM).

Akitoa hukumu ya kesi hiyo mjini Kigoma leo, Jaji wa Mahakama hiyo, Mhe.Ferdinand Wambari, amesema kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na Mlalamikaji umeshindwa kuithibitishia mahakama uhalali wa madai yaliyotolewa.

Kafulila aliwasilisha malalamiko manne ambayo ni kulalamikia utaratibu wa kuhesabu kura ambapo katika baadhi ya maeneo, msimamizi wa uchaguzi alitoa maelekezo tofauti na sheria na taratibu za uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi kushinikizwa na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya na Kamanda wapolisi wa Wilaya ili kumtangaza Hasna Mwillima kuwa mshindi.

Akitoa maelezo ya jumla ya kesi hiyo, Jaji Wambari, amesema Kafulila alishindwa kusimamia msingi wa malalamiko yake na pamoja na kuwasilisha ushahidi usio na shaka wa kusaidia malalamiko hayo ikiwemo kutowasilisha mahakamani ombi la kuitaka mahakama ihesabu upya matokeo ya vituo vyote.

Alisema pia Kafulila alishindwa kuwasilisha hati za matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi ambayo yalipaswa kulinganishwa na hati za matokeo ya vituo vyote.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Kafulila amesema hakuridishwa na hukumu hiyo ambayo amesema imeegemea upande mmoja  na kwamba anakusudia kukata rufaa kupinga maamuzi yaliyotolewa.

Nae bunge wa jimbo hilo, Hasna Mwillima, amesema Mahakama imetenda haki japo anasikitika kwamba kwamba amepotezewa muda mwingi kwani badala ya kuwatumikia wananchi wake, amekuwa akitumia muda mwingi kwa ajili ya kuhudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.