LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAAJABU: UBOVU WA BARABARA ZA MITAA KATIKA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA.

Hii ni barabara ya Sabatho-Kirumba iliyopo katika Mtaa wa Ngara, Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. Barabara hii ni imeharibika kutoka na mvua zilizonyesha Mkoani Mwanza kwa zaidi ya miezi minne iliyopita.

Wakazi wa mtaa huu wanasema, viongozi wa Serikali ya Mtaa, Kata pamoja na Manispaa, unafahamu adha wanayoipata na mara kadhaa wamekuwa wakifika kujionea barabara hiyo jinsi ilivyoharibika hivyo wanaamini itarekebishwa japo wanasikitishwa kwa namna marekebisho yake yanavyochelewa.

Ni barabara ambayo ipo mita chache kutoka Kituo cha Polisi Kirumba, ikiunganisha makazi ya wananchi kutoka jengo la chama cha waalimu mkoani Mwanza hadi kanisa la SDA Kirumba.

Chombo chochote cha usafiri hakina uthubutu wa kupita katika barabara hii. Hakika inasikitisha na ni hatari kwa maisha ya wakazi wa Kirumba.
Hii ni moja kati ya barabara mbovu zilizopo katika Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kwa ujumla hivyo tutaendelea kupachika picha zake hapa kama sehemu ya kuwakumbusha wahusika kuwahisha utekelezaji wa ukarabati barabara wa barabara hizo.
Picha na BMG.

No comments:

Powered by Blogger.