LIVE STREAM ADS

Header Ads

MACHINGA, MFUPA ULIOISHINDIKA HALMASHAURI YA JIJI MWANZA.

Ipo kauli isemayo "Mfupa Uliomshinda Fisi" ikiashiria jambo gumu mithiri ya mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyaba bingwa wa kutafuna mifupa ya kila aina.

Ndivyo unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri ya jiji la Mwanza.

Mara kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu licha ya nguvu kubwa kutumika.

Kabla ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la mwanza machinga wamezagaa ovyo.

Baadhi  ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.
Machinga wakifanya biashara katika uzio wa Msikiti wa Ijumaa, barabara ya Nyerere Jijini Mwanza
Baadhi ya maeneo ikiwemo Makoroboi, Mgambo wa jiji la Mwanza hawabanduki ili kuwazuia machinga kufanya biashara katika uchochoro wa msikiti wa Temple/Hindu ulio mkabara na shule ya awali ya Rajendra jijini Mwanza.
BMG tunajipa muda, kuona ni mkakati gani unaandaliwa ili kuwapanga tena machinga katika maeneo rasmi.
Bonyeza HAPA Kusikia Machinga Wasemavyo

No comments:

Powered by Blogger.