LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA WATISHIA MAISHA YA WAJANE MKOANI KIGOMA.

Kwa Ushonaji wa Nguo Nzuri, wasiliana nasi 0688 44 74 44 or 0767 68 38 88 tuko Ghana Green Vie Jijini Mwanza.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Wananchi katika manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma, wameliomba jeshi la polisi kuwafuatilia baadhi ya vijana wanaotambulika kwa jina la "teleza" wanao vamia makaazi ya watu na kuwabaka wanawake.

Wakitoa malalamiko yao jana katika mtaa wa Mwanga, kata ya Mwanga kusini, baadhi ya wanawake waliokwisha ingiliwa na vijana hao walisema kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakiwaingilia kimwili huku wakiwatishia kwa visu na mapanga.

Diwani wa Kata ya mwanga kusini, Mussa Maulidi, amesema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanawake waliofanyiwa vitendo vya ubakaji na kwamba wengi wao wamekuwa wakihofia kutoa taarifa kwa kuhofia kurudiwa na vijana hao (tereza) ambapo ameongeza kuwa mpaka sasa kuna zaidi ya wanawake12 waliokwisha ingiliwa kimwili na vijana hao 

Kamanda wa jeshi la polisi  mkoani Kigoma, SACP Fredinandi Mtui, amesema jeshi la polisi limepokea malalamiko hayo na kwamba kijana mmoja ambae anahofiwa kufanya vitendo hivyo anashikiliwa na polisi ili kusaidia katika upelelezi.

Hata hivyo amesema katika siku za hivi karibuni kuliibuka uvumi mitaani wa kuwepo kwa mtu anaefahamika kwa jina la Tereza ambae anajihusisha na vitendo vya kuwaingilia akina mama wajane kwa njia ya kishirikina.

Kamanda Mtui amesema baadhi ya akinamama waliokuwa wakilalamikia hali hiyo, walipokuwa wakiulizwa walikuwa wakiogopa kuelezea ukweli wa mambo ambapo tukio la jana usiku binti wa miaka 20 ameeleza kuingiliwa kimwili alipokuwa amelala.

No comments:

Powered by Blogger.