LIVE STREAM ADS

Header Ads

MANISPAA YA KIGOMA YATOA TARATIBU ZA UJENZI KWA WANANCHI WAKE.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Wakazi wa Halmashauri ya manispaa ya Kigoma,wametakiwa   kuchukua vibali vya ujenzi katika Manispaa hiyo badala ya kuchukua vibali hivyo mitaani.

Hayo yameelezwa  katika baraza la madiwani la Halmashauri hiyo, na Mwenyekiti wa kamati ya  mipango miji, ujenzi na Mazingira, Butije Hamisi, baada ya kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi na hati bandia baina ya Wakazi wa mji huo kutokana na kujenga bila kuwa na vibali vya Manispaaa.

Kila mwananchi atatakiwa kutoa shilingi 30,000 kabla ya kupatiwa kibali cha ujenzi wa Nyumba ya makazi ya kawaida na kwa Watakao jenga Ghorofa watapatiwa vibali kwa Shiringi laki tano hiyo itasaidia Wataaramu kutoa vibali baada ya kukagua lamani ya ujenzi utakao fanyika.

"Manispaa imekuwa ikitoa vibali vya ujenzi bila malipo, hivyo kupelekea  mapato halali ya vibali hivyo. Sheria hii ndogo Halmashauri itaweza kutoza ada na inatarajiwa  kuingiza mapato ya  takribani Tsh. 24,750,000 sawa na mapendekezo ya bajeti". Alisema Hamisi.

Brown Nziku ni kaimu  Mkuu wa idara ya Mipango miji na  mazingira wa Manispaa alisema Sheria hiyo itasaidia mji kujengeka kwa viwango na kupunguza  kero kwa Wananchi kuvunjiwa nyumba zao kwa kujenga maeneo ya Wazi kwa kutokuwa na vibali stahiki.

Nao madiwani wa Baraza hilo walikubaliana na sheria hiyo na kuomba  Wananchi kupatiwa vibari na maeeo halali vya kujenga ili kupunguza kero za kujenga maeneo yasiyo rasmi na kupelekea kuvunjiwa nyumba zao.

No comments:

Powered by Blogger.