LIVE STREAM ADS

Header Ads

UTPC KUISHTAKI SERIKALI.

Wakati Tanzania leo Mei 03 inaungana na Mataifa mengine duniani kuandhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC, Umesema utaifikisha Serikali Mahakamani kutokana na mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi alieuawa akiwa kazini Mkoani Iringa.
Imeandaliwa na BMG

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan (Pichani), alitoa kauli hiyo jana, wakati akichangia Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lililofanyika jana Jijini Mwanza.

Karsan alisema aliesababisha kifo cha Mwangosi alikuwa ni mtumishi wa Serikali hivyo lazima serikali iwajibike katika mauaji hayo ikiwemo kutoa fidia kwa familia ya marehemu mwangosi ambae enzi za uhai wake alikuwa Mwandishi wa Habari wa Chanel 10 na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa.

Dunia inaadhimisha siku hii ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lengo likiwa ni kushinikiza Mataifa mbalimbali duniani kuwa na sheria rafiki za Vyombo vya Habari na hata kukemea matendo yasiyo mema ambayo wanahabari wamekuwa wakikumbana nayo wakiwa nje ama ndani ya majukumu ya kazi. Hata hivyo mambo hayo bado yanaonekana changamoto kutekelezwa.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lililofanyika jana Malaika Beach Resort Jijini Mwanza
Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016, Kitaifa yanafanyika Mkoani Mwanza ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande huku wageni mbalimbali wa heshima akiwemo Waziri wa Habari Mhe.Nape Moses Nhauye wakitarajiwa kuhudhuria.

No comments:

Powered by Blogger.