LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI ANATEKELEZA SERA YA CCM KWA VITENDO.

Msafara wa Mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, baada ya kuwasili katika Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Na Fahadi Siraji, Same 

Umoja wa Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema mambo yote yanayofanywa  na Rais Dk.John Pombe Magufuli toangu aingie madaraka yanatokana na misingi ya  sera, shabaha na malengo ya Ilani ya uchaguzi ya wa chama hicho ya mwaka 2015/2020.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo Taifa, Shaka Hamdu Shaka, ameyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Stendi Kubwa Wilaya ya Same Mashariki Mkoani Kilimanjaro.

"Iko wapi hiyo inayoitwa ilani ya uchaguzi ya upinzani, sikumbuki kama wana ilani ya uchaguzi. Nijuavyo wana shehena ya magunia ya matusi, jeuri na ubabaishaji si Ilani kama ile ya CCM. Alieleza Shaka ambae ahakukubaliana na baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanaosema Rais Magufuli anatekeleza ilani ya vyama vyao.

Shaka alisema dhamira alionayo Rais Dk Magufuli ni kuhakikisha anarudisha heshima ya serikali, kuleta mageuzi ya kiutendaji katika maeneo ya kazi, kupambana na wahujumu uchumi.
Wanaccm Wilayani Same wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kukubaliana na hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.
Umati wa wananchi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ukimpokea kwa Shangwe na Nderemo.
Wanachama wapya  wakila kiapo cha chama  na Jumuiya katika kikao cha ndani kilicho fanyika katika Wilaya ya Same Magharibi
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka Akihutubia Umati wa wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi kadi kwa wanachama Wapya 
Kaimu Katibu MkuuUVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akikabidhi kadi chipkizi mara baada ya kuwasiri katika viwanja vya Stend Kubwa 
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka (Kushoto) akimkabidhi kadi ya Chama cha mapinduzi, aliekuwa Mgombea udiwani Kata ya Kisima wilayani Same kupitia CHADEMA.
Kaimu Katibu MkuuUVCCM Taifa Shaka Hamdu Shakaakionyesha kadi mara baada ya kuzipokea.
Mwenyekiti Wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Juma Raibu Akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu Kuzungumza na wananchi
Kaimu Katibu MkuuUVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akihutubia Wananchi wa Same katika mkutano wa hadhara.

No comments:

Powered by Blogger.