LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBUNGE VITI MAALUMU MKOANI IRINGA KUWAPIGA MSASA WANAWAKE.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Iringa, Rose Twelve, akifurahi jambo na akinamama wenye ulemavu Mkoani humo.

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve akizungumza na wanawake wa chama cha mapinduzi ccm mkoani iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Wananchi Mkoani Iringa wanatarajia kunufaika na Muungano wa Wabunge Watatu Vijana wa Viti Maalumu Mkoani humo, kwa lengo kubadilishana uzoefu wa kuwaletea Maendeleo Wanawake Mkoani Iringa.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Iringa, Rose Twelve, amesema wameamua kuungana ili kubadilisha mfumo wa utawala na kuondoa ufanyaji wa kazi kwa mazoea sambamba na kuwasaidia wananchi wanaowatumikia.

“Unajua kuwa changamoto na matatizo ya wanawake kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo najifunza kwa wenzangu wanatatuaje changamoto hizo ili na mimi niweze kutatua matatizo ya wanawake wa mkoani iringa na waendelee kufanya maendeleo huku wakiwa hawana changamoto nyingi”. Alisema Rose

“Nitatoa milioni hamsini kila mwaka kwa umoja wa Wanawake wa CCM UWT Mkoani hivyo lazima nitafute njia mbadala ya kuwapa elimu ya kuzitumia hizo pesa ili ziwanufaishe kwa kuwaletea maendeleo”.alisema Rose

Rose alisema kuwa atatafuta wataalamu wa mafunzo mbalimbali ili wanawake wa Mkoa wa Iringa wapate elimu ya ujasiriamali na kuokoa pesa ambazo zimekuwa zikipotea.

"Nitatafuta wadau mbalimbali wachangie mfuko wangu wa mbunge kwa lengo la kuwasaidia wanawake ambao hawana mitaji ya kujiendesha maisha yao". Alisema Rose huku akiwataka wakazi wa Iringa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

No comments:

Powered by Blogger.