LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAKRIBANI WAKAZI 40,000 KATIKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA WANUFAIKA NA MV.JUBILEE HOPE.

Wagonjwa wakiwa wanasubiria huduma ndani ya MV. Jubilee Hope kisiwa cha Goziba Muleba.
Judith Ferdinand, Mwanza
Wakazi zaidi ya 39,000 wanaoishi kwenye Visiwa vya Ziwa Victoria katika Wilayani Muleba mkoani Kagera, wamenufaika na mradi wa meli ya matibabu wa Mv.Jubilee Hope, unaoendeshwa na Kanisa la Afrika Inland Church Tanzania (AICT), Dayosisi ya Geita chini ya shirika la Vine Trust lililopo Scottland  nchini Uingereza.

Mkurugenzi wa mradi huo, Emmanuel Njabugeni, amesema mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano pia na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kuhudumia visiwa vilivyopo wilayani humo, ambavyo ni vingi na vipo mbali ambapo huduma za afya na jiografia yake hafikiki kwa urahisi.

Njabugeni mesema katika kisiwa cha Goziba, februari mwaka huu waliweza kuwa hudumia wagonjwa 27 waliougua ugonjwa wa kipindupindu na kati ya hao 24 walipona, 4 walipoteza maisha kutokana na kuwa na hali mbaya.

No comments:

Powered by Blogger.