LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAFUNZI WALIOSOMA LORETO SEKONDARI MKOANI MWANZA WAKABIDHI MSAADA SHULE YA WALEMAVU MITINDO.


Judith Ferdinand, Mwanza
Wananchi, Serikali  pamoja na wadau mbalimbali nchini, wametakiwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, chakula na malazi, ili waweze kufikia ndoto zao.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari ya Wasichana Loreto (LORETO ALUMNI), mkoani  Mwanza, Pamela Felix, ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi msaada mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Umoja huo kwa wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Mitindo iliyopo Wilayani Misungwi ambayo ni shule inayotoa elimu maalumu kwa wanafunzi wenye ulemavu.

"Kwa kuwa huu ni mwaka wa huruma kwa dhehebu la Romani Katoliki,  tumeona  ni bora  kufanya matendo ya huruma kwa watu wengine ikiwemo kuwasaidia watoto walio katika kituo hiki cha Mitindo, kucheza nao pamoja na kuwasaidia mahitaji mbalimbali", alisema Felix.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Shule hiyo, Christopher Mihayo ambae ni mwalimu wa Elimu Maalumu upande wa Viziwi shuleni hapo, amesema kuna baadhi ya wazazi wanapowafikisha watoto katika shuleni hiyo, huwa hawarudi tena kuwatembelea wala kuwafuata wakati wa likizo jambo ambalo hutafsirika kama vile wamewatelekeza watoto wao.

No comments:

Powered by Blogger.