LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAJETI YA TANZANIA KWA MWAKA 2016/17 YALENGA KUBORESHA ZAIDI MAISHA YA WANANCHI.


Kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, imewasilisha bajeti yake ya mwaka 2016/17 ambapo bajeti hiyo imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 ikilinganishwa na bajeti inayomalizika.

Akiwasilisha bajeti hiyo hii leo bungeni mjini Dodoma, Dkt.Mpango amesema kuwa jumla ya bajeti ya mwaka 2016/17 ni shilingi trioni 29.54 ambayo ni ongezeko la jumla ya shilingi tirioni 7.04 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2015/16 ya shilingi tirioni 22.49 ambapo katika bajeti hiyo, matumizi ya kawaida ni trilioni 17.7, mikopo ni trilioni 11.1.

Bajeti hiyo imewasilishwa sambamba na kaulimbiu yenye lengo la “kuongeza uzalishaji viwandani ili kupanua fursa za ajira” huku ikiwa na mikakati ya kuboresha maisha ya kila mtanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi wa viwanda, afya, elimu, miundombinu ya uchukuzi, umeme pamoja na maji.

Pia mapendekezo katika majeti hiyo yamelenga kupunguza kodi ya ongezeko la thamani kwenye mbogamboga zote pamoja na mazao ya mifugo kabla ya kusindikwa huku ikilenga kuongeza ushuru wa bidhaa unaotozwa kwenye samani zinazoagizwa nje ya nchi kutoka asilimia 15 hadi 20 ili kuhamasisha matumizi ya samani zinazotengenezwa kwa kutumia mbao zinazozalishwa hapa nchini, kuongeza ajira na kuongeza mapato ya Serikali.
BMG

No comments:

Powered by Blogger.