CITY FM RADIO YA JIJINI MWANZA YAZINDUA KAMPENI YA KUZUIA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI.
Radio City Fm ya inayomilikiwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza, jana imezindua Kampeni ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuepuka matumizi ya Mifuko ya Plastiki ambayo ni hatarishi katika uchafunzi wa Mazingira na kuhimiza zaidi matumizi ya mifuko mbadala ikiwemo vikapu vya asili katika shughuli mbalimbali ikiwemo mahemezi sokoni.
Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa City Fm wakiwa pamoja na maafisa Mazingira kutoka halmashauri ya jiji la Mwanza, wakitoa elimu ya kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki katika mtaa wa Tanganyika Bus ikiwa ni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki.
Katika Uzinduzi huo, kulikuwa na mifuko/ vikapu mbadala ambavyo City Fm ilikuwa ikivitoa kwa wananchi waliokuwa wakifanya mahemezi yao ili kuwafanya watambue kwamba kuna mbadala wa mifuko hatarishi ya plastiki katika kufanya mahemezi yao.
Kampeni hiyo imezinduliwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira ambayo huadhimishwa kila mwaka kuanzia June Mosi hadi June Tano. Uzinduzi wake ulikuwa ukiruka moja kwa moja hewani kupitia 90.2 City Fm Mwanza.
Mmoja wa akina mama akipewa kikapu kwa ajili ya mahemezi baada ya kukutwa Soko Kuu la Jijini Mwanza akifanya mahemezi kwa kutumia mifuko hatarishi (ifuko ya naironi/mifuko ya rambo).
Baada ya mahemezi, ukafuata wasaa wa elimu kutolewa
Mama Lilian Josephat baada ya kupokea elimu juu ya kuepuka matumizi ya mifuko ya plastiki, aliiomba serikali kuzuia uzalishaji wa mifuko hiyo kwa kuwa elimu pekee haitoshi wakati uzalishaji wa mifuko hiyo unaendelea kwa kasi.
Mmoja wa wafanyabiashara wa mifuko ya rambo akitazama kikapu ambacho ni mbadala wa matumizi ya mifuko ya plastiki na kusema kuwa ni vyema uzalishaji wa mifuko hiyo ukakoma ili matumizi ya vikapu katika mahemezi yapewe kipaumbele zaidi kwa kuwa hayana adhari katika mazingira.
Muuzaji wa mifuko ya rambo akisikitika kwamba biashara yake sasa imeingiliwa.
Wananchi wakitoa maoni yao juu ya kusitishwa kwa matumizi ya mifuko ya rambo/ plastiki ambapo wanasema itakuwa kazi ngumu kusitisha matumizi ya mifuko hiyo ikiwa viwanda vitaendelea kuizalisha kwa kuwa, upatikanaji wake ni wa haraka na inauzwa kwa bei nafuu ya shilingi mia moja, mia mbili ama mia tano ikilinganishwa na vikapu ambavyo huuzwa kuanzia shilingi elfu moja mia tano.
Elimu ya kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki ikiendelea kutolewa kwa wananchi katika mtaa wa Market Street uliopo Soko Kuu Jijini Mwanza.
Mjasiriamali wa kuuza mahindi nae akapewa elimu juu ya madhara yanayotokana na kufunika mahindi kwa kutumia mifuko ya plastiki/ rambo
Elimu ya kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki ikiendelea kutolewa kwa wananchi katika mtaa wa Market Street uliopo Soko Kuu Jijini Mwanza.
Ikabidi mama apewe pesa ili akanunue ndoo kwa ajili ya kufunikia mahindi yake badala ya kutumia mifuko ya rambo na kuhatarisha afya ya mlaji.
Elimu ya kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki ikiendelea kutolewa kwa wananchi katika mtaa wa Market Street uliopo Soko Kuu Jijini Mwanza.
Matumizi ya mifuko ya rambo ni makubwa sana katika jamii
Matumizi ya mifuko ya rambo ni makubwa sana katika jamii
Robo tatu ya wananchi katika umati huu uliopo Soko Kuu la Jijini Mwanza, wanatumia mifuko ya plastiki/ rambo katika mahemezi yao.
Baada ya matumizi, mifuko ya rambo/ mifuko ya plastiki huwa ni hatari katika mazingira kwa kuwa haiozi na hata ukiichoma huzalisha hewa chafu na hatari kwa viumbe hai na mimea.
My Bag Campaign, Zuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki yasiyo Rafiki wa Mazingira.
Charles Aman ambae ni Afisa Mazingira, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, akizungumza katika uzinduzi wa My Bag Campaign
Desderius Polle ambae ni Meneja dampo la Buhongwa jijini Mwanza, akizungumza katika uzinduzi wa My Bag Campaign
Iman Hezron kutoka City Fm ambae pia ni mratibu wa My Bag Campaign, akizungumza katika uzinduzi wa My Bag Campaign.
Imeandaliwa na BMG
No comments: