LIVE STREAM ADS

Header Ads

DIWANI WA KATA YA ILEMELA JIJINI MWANZA APANIA KUIBADILI KATA HIYO.


Judith Ferdinand, Mwanza
Diwani wa Kata ya Ilemela iliopo katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Willbard Kilenzi, ametoa ahadi ya kuchangia vifaa  mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kata hiyo.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka katika kata hiyo, ulioandaliwa na diwani huyo kwa ajili ya kujadili changamoto zinazoikabiri Kata hiyo na namna ya kuzitatua.

Kilenzi aliahidi kuchangia lori nne za mawe, huku akiwataka wadau hao kukamilisha ahadi zao hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu ili siku ya sabasaba waweze kuzindua ujenzi huo kwa wananchi kushiriki kwenye uchimbaji wa msingi.

Pia aliwaomba wenyeviti wote wa mitaa iliopo ndani ya kata hiyo, kuwahamasisha wananchi kushiriki na kuchangia katika shughuli za maendeleo, kwani serikali pekee haiwezi.

Hata hivyo alisema ameamua kuwashirikisha wadau hao kutokana na  zahanati ya kata hiyo, kuwa na chumba kimoja kinachotumika kutolea huduma ya uzazi wa mpango,kujifungua kwa wajawazito sambamba na kuwapumzishia watoto waliozaliwa pamoja na mama zao,hali ambayo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto.

Kwa upande wake mmoja wa wadau hao Richard Peter, alimuomba diwani  kuzungumza na wawekezaji waliopo ndani ya kata hiyo, ili waweze kuchangia na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Naye Charles Lukala alisema, ili kupata maendeleo katika maeneo mbalimbali, wananchi lazima wajitoe kwa kuchangia pamoja na kushirikishwa katika masuala ya kimaendeleo.

Alimuomba diwami wa Kata hiyo pamoja na wananchi kushirikiana ili kuandaa kongamano ambalo watawaalika viongozi mbalimbali na kuchangisha fedha zitakazofanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata yao.

No comments:

Powered by Blogger.