HABARI NJEMA KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Nasi Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Mchungaji Dr.Daniel Moses Kulola (Kushoto) na Mama Mchungaji Mercy Daniel Moses Kulola (Kulia).
Kanisa la
EAGT Lumala Mpya lililopo Soko Jipya la Sabasaba, Ilemela Jijini Mwanza chini
ya Mchungaji Dr. Daniel Moses Kulola, linawakaribisha
watu wote kwenye ibada zake, ambapo wenye kusumbuliwa na nguvu za giza, majini,
uchawi, ndoa zenye misukosuko, kukosa mafanikio katika biashara, kukosa ajira,
kushindwa masomo pamoja na wenye kukosa mafanikio maishani, wataombewa BURE
kabisa.
Kumbuka
Mchungaji Dr.Daniel Moses Kulola ambaye ni mtoto wa aliekuwa Askofu Mkuu wa
Makanisa ya EAGT, hayati Dr.Moses kulola, amefundishwa na kulelewa vyema na Mzee
Kulola, amejipanga vyema na timu yake kukuhudumia kupitia maombezi na kwa Jina
la Yesu, UTAFUNGULIWA.
Yapo
mafanikio kupitia maombezi hivyo hakikisha unafika kwenye ibada za Kanisa la
EAGT Lumala Mpya kila jumapili ambapo ibada ya kwanza inaanza saa saa 07:00
hadi 10:15 asubuhi na ibada ya pili inaanza saa 10:30 asubuhi hadi 02:00 alasiri.
Katika ibada
hizo, Kwaya mashuhuri za Havillah, Revival na Hot spears zitakudumu, huku waimbaji
wenye nguvu ya Mungu kama Sarah Emanuel, Happy Shamawere, Theo Dave, Agnes
Akrama, Ndangeji, Mitagato pamoja na Abuu Levy nao pia wakihudumu katika ibada
hizo.
Usithubutu
kwenda kwa Waganga wa kienyeji na badala yake fika katika Kanisa la EAGT Lumala
Mpya ambapo kuna Kuinuliwa na Uponyaji kwa Jina la Yesu.
Ili kufika katika Kanisani la EAGT Lumala Mpya, panda
magari ya Airport au Ilemela, shuka kituo cha Sabasaba kona ya Kiseke, uliza
bodaboda wapi lilipo Kanisa la Mchungaji Dr.Daniel Moses Kulola watakuonyesha,
ama tembea hatua chache hadi Soko Jipya la Sabasaba na nyumba ya soko hilo
utaona Kanisa Kubwa lenye rangi nyeupe.
Kwa Msaada wa Kiroho, wasiliana na
Mchungaji Dr.Daniel Moses Kulola kwa nambari za simu 0767 74 90 40.
Bonyeza Hapa Kusikiliza Au Bonyeza Play Hapo Chini
Bonyeza Hapa Kusikiliza Au Bonyeza Play Hapo Chini
No comments: