LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALMASHAURI YA USHETU MKOANI SHINYANGA MATATANI.


Na Shaban Njia
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini matumizi mabaya ya fedha katika halmashauri ya Ushetu iliyopo katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Hayo yameelezwa katika kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Ushetu,  kilichohudhuriwa pia na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, John Mongela, kilichokuwa na lengo la kujadili hoja za za ripoti ya CAG ambapo kilijumuisha pia madiwani wa halmashaur hiyo pamoja na Wakuu wa Idara.

Ripoti hiyo ya CAG ilibaini kwamba Halmashauri ya Ushetu ilibainika kuwa haiko madhubuti katika kusimamia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mongella, aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kuhakikisha kwamba wanasimamia vyema shughuli za maendeleo ikiwemo ukusanyaji wa kodi huku akimtaka Isabela Chilumba ambae ni mkurugenzi katika halmashauri hiyo kumwandikia barua ya onyo mkaguzi wa ndani wa halmshauri hiyo kutokana na kushindwa kubaini mapungufu katika halmshauri yake.

No comments:

Powered by Blogger.