LIVE STREAM ADS

Header Ads

JIJI LA MWANZA BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Nasi Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Magari ya kuzoa Uchafu/Taka yakizoa uchafu/Taka katika dampo lililopo Soko Kuu Jijini Mwanza. Damo hili awali lilikuwa likiwapa kero kubwa wafanyabiashara wa Soko Kuu Jijini Mwanza pamoja na wateja wao kutokana na uchafu/taka kukaa muda mrefu bila kuondolewa hali ambayo sasa ni tofauti kwani uchafu/taka umekuwa ukiondolewa kwa wakati.
Juhudi ziendelee kuongezeka ili uchafu uwe unaondolewa haraka katika eneo hili pamoja na maeneo mengine ya kukusanyia uchafu (Madampo) jijini Mwanza ili kuimarisha hali ya usafi zaidi maana sifa kubwa ya Jiji la Mwanza kwa miaka mingi ni USAFI.

Pia zoezi la kufanya usafi kwa watu wote kila jumamosi ya mwisho wa mwezi liendelee kupewa mkazo ili kila mmoja katika jamii na eneo lake la biashara atambue umuhimu wa kuimarisha usafi. Wananchi nao wazingatie matumizi ya vyombo vya kukusanyia uchafu katika maeneo yao pamoja na vile vilivyosambazwa takribani mitaa yote Jijini Mwanza. BMG inatoa pongezi za dhati kwa uongozi wa halmashauri jijini Mwanza, uliopo na uliopitia kwa kuimarisha Usafi katika mitaa yake.
Mwanza Bila Uchafu Inawezekana!

No comments:

Powered by Blogger.