KUKU PORI.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Hakuna Uthibitisho wa moja kwa moja kwamba ndege hawa wanaliwa ama la!
Ila George Binagi-GB Pazzo amekutana nao Jijini Mwanza na ikamjia kumbukumbu ya miaka mingi iliyopita wakati akiwa mdogo ambapo aliwahi kusafiri kwenda Jijini Dar es salaam na alipofika mkoa fulani akakuta watu/ abiria wanakula nyama ya kuku ambao walikuwa wakubwa kweli kweli.
Alipojaribu kuuliza kuhusiana na aina ya kuku hao, abiria mmoja akamtania kwamba hao ni 'Kuku Pori" kama walivyozoeleka kuitwa kwa jina la Bwana Afya wa Porini ama Ekemera Nchoka kwa lugha ya Kikurya.
BMG inakuacha na swali; Je ndege hawa wanatumika kama kitoweo?
No comments: