LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADAKTARI KANDA YA ZIWA WAJENGEWA UWEZO WA KUFANYA TATHMINI KUTOKANA NA AJALI KAZINI.


Judith Ferdinand, Mwanza
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameshiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini ya magonjwa, ajali na vifo, visababishwavyo na ajali kazini.

Akizungumza jana mkoani jijini Mwanza katika ufunguzu  mafunzo hayo ambayo ni ya siku tano, yaliyoandaliwa na  Mfuko wa Fidia  kwa Wafanyakazi (WCF) na  kudhaminiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi  na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, alisema kupitia semina hiyo, washirki wataweza kutoa ushauri unaostahili kuhusu ulipaji fidia kwa wanaostahili pamoja na kufahamu sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008.

Isaka alisema, matarajio yao  ni kwamba mafunzo hayo yatawezesha mfuko kutekeleza jukumu la kufanya tathmini kwa wakati kuhusu magonjwa yatokanayo na kazi, hali itakayosaidia kuondoa changamoto zilizokuwepo kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo.

Pia alisema, kupitia mfuko huo uchumi wa nchi utakua sambamba na kuboresha maisha ya wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi, kutokana na kulipwa hadi asilimia 70 ya mshahara wa mtu aliye pata ajali tofauti na zamani ambapo malipo yalikuwa ni 100,008 ikizingatia sasa gharama za matibabu ni kubwa.

Aidha aliongeza kwamba, ili kuwaondolea gharama waajiri kulipa katika mifuko mingi ya hifadhi ya jamii na makato makubwa kwa wafanyakazi, mamlaka itafanya tathimini ya fedha inayochangiwa katika mifuko hiyo na kuigawanya kiasi kuingia katika mfuko huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, alisema uwepo Wa mfuko huo ni hatua ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili wafanyakazi, kwani utatoa mafao mbalimbali ikiwemo  matibabu, malipo ya amayemhudumia magonjwa, ulemavu wa muda na kudumu, huduma za ukarabati na ushauri nasaha pamoja malipo kwa wategemezi endapo muhusika atafariki akiwa anatekeleza majukumu ya mwajiri wake.

Naye Mkurugenzi Mkuu Wa WCF, Masha Mshomla, alisema, mfuko huo unatoa fidia kwa walio umia katika mazingira ya kazi tofauti na mifuko mingine inayotoa huduma kwa muda mrefu kama mtu akistaafu na kupoteza maisha.

Pia alisema, watashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo madaktari, waajiri, wataalamu wao pamoja na polisi ili kusaidia kupata uhakika  na kufahamu mazingira ya ajali ilivyo tokea,maeneo ilipotokea na alichokuwa anafanya.

No comments:

Powered by Blogger.