USAILI WA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAISHA PLUS 2016 MKOANI MTWARA NI NOMA SANA.
Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya Maisha Plus imeanza rasmi jumamosi June 04,206 kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel ya NAF Beach iliyoko Mtwara ambapo Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia walijitokeza.
"Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana, niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
- Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara. Mshiriki Grace Pemba anaelezea changamoto mbalimbali alizokutana nazo kutokana na kuolewa akiwa na umri mdogo, anasema hadi sasa ana watoto wawili ambao wanaishi na baba yao. Alipoulizwa maswali zaidi Grace alijawa na simanzi na kujikuta akitoa machozi, "Nimelia kwa sababu mmenikumbusha nyuma nilikotokea" anasema Grace mfanyakazi wa Saloon kutoka mkoani Mtwara.
- Waandaaji wa mashindano ya Maisha Plus wakibadili utaratibu wa awali wa kupiga picha baada ya maji kujaa.
Muhitimu wa shahada ya kilimo William Mbaga alibanwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo faida za kilimo cha 'greenhouse' pamoja na namna ambavyo maziwa ya mtindi yanapatikana. William alijieleza kwa ujasiri.
- Waigizaji pia walikuwemo katika usaili wa #MaishaPlusMtwara
- Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
"Mwaka huu washiriki wajipange sana. Maandalizi yaliyofanywa kufanikisha msimu huu hayajawahi kutokea katika historia ya Maisha Plus. Ni kama tunaanza moja" Alisema Masoud Kipanya, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa mashindano haya.
"Tumewekeza katika teknolojia ya kisasa ili kupata picha za matukio yenye uhalisia zaidi. Watazamaji wategemee burudani safi isiyomithirika kupitia Azam Two." Alisema David Sevuri, miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus. Taarifa mbalimbali kuhusu mashindano haya zinapatikana kupitia tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv
No comments: