LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAFURIKO YA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WASHUHUDIA TUNGURI ZIKITEKETEZWA KATIKA MKUTANO WA INJILI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Nasi Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Maelfu ya Wakazi wa Jiji la Mwanza wameendelea kumiminika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza kushuhudia Mahubiri ya Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Ujerumani, Daniel Kolenda, anaehubiri katika Mkutano wa Reinhard Bonnke, ambao umeandaliwa chini ya huduma ya Kimataifa ya "Christ For all Nations" kwa ushirikiano na Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza.

Watu wengi wamepokea uponyaji katika Mkutano huo ambao ulianza June 23,2016 huku ukitarajia kufikia tamati leo June 26,2016. Wengi wameokoka huku wengine wakisalimisha tunguri zao walizokuwa wakizitumia katika shughuli za giza kwa ajili ya kuteketezwa moto baada ya kumpokea Kristo.
Maelfu ya Wakazi wa Jiji la Mwanza, wakifuatilia Mahubiri katika Mkutano wa Injili unaofanyika katika Uwanja wa Furahisha.
Watumishi wa Mungu wakihudumu katika Mkutano huo
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Ujerumani, Daniel Kolenda (kulia), akihubiri katika Mkutano Mkubwa wa Injili unaofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza. Kushoto ni mkarimani wake.
Watumishi wa Mungu wakihudumu katika Mkutano huo
Watumishi wa Mungu, wakiongozwa na Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza, Zenobius Isaya (katikati) wakihudumu katika mkutano huo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, John Lissu (wa kwanza kushoto) pamoja na waimbaji wengine wakihudumu katika mkutano huo.
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakihudumu katika Mkutano huo
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakihudumu katika Mkutano huo
Watumishi wa Mungu wakiwa katika mkutano huo
Waliookoka walipewa vitabu kwa ajili ya kujisomea ili wajijenge zaidi kiroho
Tunguri za Wachawi zikiteketezwa katika mkutano huo. Ni baada ya wachawi na washirikina kumpokea Kristo na hivyo kusalimisha tunguri zao.

No comments:

Powered by Blogger.