LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMBO MACHACHE NA MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU ROCK CITY MALL MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Nasi Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Hili ni jengo la Soko la Kimataifa lililopo Jijini Mwanza. Linajulikana zaidi kwa jina la Rock City Mall. Ni soko kubwa kuliko yote Afrika Mashariki. Soko hili lina ukubwa wa mita za mraba 48,250 huku likiwa na eneo la maegesho ya magari 600, pikipiki na baiskeli 150, eneo la michezo ya watoto mita za mraba 15,200 na hivyo kufanya eneo lote la Rock City Mall kuwa mita za mraba 71,990.

Rock City Mall inafuatiwa na Soko la Mlimani City lililopo Jijini Dar es salaam lenye mita za mraba 11,500 ambalo ni soko kubwa Afrika Mashariki lililochukua nafasi ya pili kwa ukubwa baada ya lile la nchini Kenya la Westgate kuvamiwa. Westgate ilikuwa na ukubwa wa mita za mraba 30,000.

Mbali na ubunifu na uzuri wa jengo, ukifika Rock City Mall utafurahi kupata kila aina ya mahitaji. Kuna huduma na maduka ya kila aina na bado uwekezaji unaendelea kufanyika. Lakini kwa waandaaji wa matamasha hapa ndipo mahali pake. Hakika Jiji la Mwanza pamoja na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), wanastahili pongezi kwa kufanikisha mradi huu mkubwa.
Mdau katembelea Rock City Mall
Mdau na Mapozi yake
Mdau kwa raha zake, akiangalia wanaokuja na wanaokwenda
Rock City Mall
Leo tumeishia kutazama mandhari ya nje, wakati mwingine tutaingia ndani kujionea mandhari ilivyo. Bila shaka nawe unajiandaa kufika Rock City Mall, ila ukishindwa kufika basi BMG itapachika hapa picha ili utazame mandhari yake.

No comments:

Powered by Blogger.