LIVE STREAM ADS

Header Ads

MCHUNGAJI WA KIMATAIFA ALIEFARIKI NA KUFUFUKA SIKU YA NNE ATOA RAI KWA WATANZANIA.


Ujumbe wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manisapaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ukiongozwa na Mchungaji wa Kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola (Wa Pili Kushoto), ukiwa katika Uwanja wa ndege Jijini Mwanza kwa ajili ya kumpokea Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Canada, Mama Domitila Nabibone (Wa tatu kushoto), aliefika Jijini Mwanza kwa ajili ya Mkutano Mkubwa wa Open Your Eyes and See (OYES 2016) unaofanyika katika Kanisa hilo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Watanzania wametakiwa kuacha kutenda matendo maovu na  badala yake watende matendo yanayompendeza Mwenyezi Mungu, ili kupata kibali cha kuuona ufalme wa mbinguni.

Mchungaji wa  Kimataifa wa Kanisa la Ark of The Lord Temple lililopo Ottawa nchini Canada, Domitila Nabibone, aliyasema hayo jumapili iliyopita baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege jijini Mwanza kwa ajili ya  mkutano wa injili wa Open Your Eyes and See (OYES 2016), ulioandaliwa na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela mkoani Mwanza.

Mch.Nabibone alisema ili kuuona ufalume wa mbingu, jamii inatakiwa kuacha dhambi na kuishi kwa kushika sheria za Mungu pamoja na kutenda matendo mema wakati wote.

Alitanabaisha kwamba kuna tofauti kubwa kati ya dini na wokovu na kwamba watu wengi wamekuwa wakisali tu lakini matendo wanayofanya hayampendezi Mwenyezi Mungu.

Alidokeza kuwa aliagizwa na Mungu kuja kuwahubiria wanadamu ulimwenguni neno lake ili waache kutenda dhambi na kumfuata yeye, baada ya  mwaka 1968 akiwa nchini Congo kufariki kwa siku tatu na siku ya nne kufufuka.

"Watu wajue Mungu yupo na mbingu ipo, kwani mambo nilioonyeshwa yanashangaza, hivyo nilirudishwa duniani ili kuwasimulia wasio muamini Yesu ili wamuamini na waache dhambi". Alisema Mchungaji Nabibone.

No comments:

Powered by Blogger.