LIVE STREAM ADS

Header Ads

THAMANI YA KUONA VYEMA KIROHO.

Mchungaji Methew Alex anaehudumu nchini Uingereza, akihudumu katika Ibada ya Jumapili June 12,2016 katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Alifundisha juu ya "Thamani ya Kuona Vyema Kiroho". Alisema tatizo kubwa la watakatifu ni kushindwa kuona kiroho na kutambua wao ni akina nani. Wanatembea huku wakijiona mioyoni mwao kuwa wao ni dhaifu na hivyo ndivyo maisha yao yanavyokuwa dhaifu kweli.

"Unapaswa kuona kwa tofauti ukiwa na Mamlaka ya Mungu ili hata pepo akikuona atetemeke na kushindwa kukusogelea katika jina la Yesu. Ukiangalia kwa wasiwasi, moyo wako nao utajawa na hofu na mdomo wako utanena kwa hofu na hatimae utashindwa kufanikiwa maishani mwako". Anasema Mchungaji Alex.

Ni vyema kuona vizuri kiroho. Ukiona umaskini moyoni mwako, utaishia kuwa maskini. Angali katika ushindi nawe utakuwa mshindi. Hata kama umekulia katika umaskini, angalia katika utajiri na utakuwa tajiri. Mungu anaingia mkataba na watu wenye maono mema. Mungu afungue macho yako na uone Baraka zako kwa jina la Yesu, Amina.

Kwa muda wako, soma maandiko yafuatayo; Mwanzo 13:14, Yeremia 29:11, 2-Wafalme 6:17 na 1-Wakorintho 2:10.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, wakiwa katika Ibada ya ya jumapili June 12,2016 iliyoongozwa na Mchungaji Methew Alex anaehudumu nchini Uingereza.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, wakiwa katika maombezi katika Ibaya ya jumapili June 12,2016 iliyoongozwa na Mchungaji Methew Alex anaehudumu nchini Uingereza.
Imeandaliwa na BMG

No comments:

Powered by Blogger.