LIVE STREAM ADS

Header Ads

NG'OMBE ZILIZOKAMATWA KATIKA PORI LA MUOWISI KIGOSI MKOANI GEITA ZAPIGWA MNADA.


Na Shaban Njia
Zoezi la kutoa mifigo ikiwemo ng’ombe katika pori la akiba la Muowisi Kigosi lililopo katika mikoa mitano Kanda ya Ziwa na Magharibi ina lengo la kuifanya mikoa hiyo kuwa na vivutio vya utalii vitakavyoinufaisha mikoa hiyo kwa miaka mitano ya baadaye.

Akiongea na waandishi wa habari siku moja  baada ya kufanya zoezi la uuzaji wa ng’ombe 494 waliokamatwa katika pori hilo mwezi wa tatu mwaka huu, Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Muowisi Kigosi mkoani Geita, Iman Mkonda, alisema kuwa zoezi hilo  litakuwa endelevu.

Mkonda alisema kuwa pori hilo ambalo linaunganisha Mikoa mitano ya Kigoma, Shinyanga, Kagera, Geita na Tabora yenye vivutio vingi vya utalii likiwa ni pori la pili hapa nchini ukiacha lile kubwa la Seluu lililopo kati ya Mikoa ya Iringa na Morogoro.

Alisema katika Minada tofauti ya kuwauza ng’ombe hayo walioingia katika pori hilo bila ya kupata vibali ilifanyika kwa nyakati tofauti katika Vijiji vya Nyarwerwe wilayani Kahama, Kijiji Mdendele wilayani Bukombe na wilayani Geita ambapo zaidi ya shilingi milioni 234 zilipatikana baada ya ng'ombe 494 kununuliwa.

Aliwataka Wananchi kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi hiyo ili kutunza uhifadhi wa mazingira kwani wanyama wamekuwa wakihama hama kutoka na shughuli za kibinadamu zinzofanyika katika Pori hilo na kutishia kutoweka kwa baadhi ya wanyama.

No comments:

Powered by Blogger.