TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN KARATE.
Mwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza la OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" lenye makao Okinawa nchini Japan, juzi alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu magwiji wa karate lilifanyika Lisabon nchini Ureno.
Na MtazamoMedia
Na MtazamoMedia
Magwiji wa karate duniani wakiwa katika picha ya pamoja katika kongamano la Karate European Jundokan Gasshuku.
Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza
la OKINAWA
BODOKAN & KARATE FEDERATION" lenye makao Okinawa nchini Japan, juzi alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu
magwiji wa karate lilifanyika Lisabon nchini Ureno.
Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la dojo iliyo
jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha,
Okinawa baada ya kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu ,
Master Chijun Miyagi , ambayo hivi sasa inaendeshwa na mtoto wake
Yoshihiro Kancho Miyazato.
Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama
mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa
chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.
Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate " European Jundokan Gasshuku 2016".
Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa
sanaa asili ya mitindo ya karate toka Okinawa kiitwacho".
"OKINAWA
BODOKAN & KARATE FEDERATION" imefanya mabadiliko hivi karibuni
yatakayo tofautisha karate asilia na ile ya kimichezo itayo kuwa
katika michezo ya Olympics.
Kutokana na mabadiliko ya kimbinu na ufasaha yanayo onekana
katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi
karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.
Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba mbinu halisi,
zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya karate toka visiwani
Okinawa duniania kote.
Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka
mitindo mbalimbali inayo tambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa
mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa inafundisha na waasisi wake asilia.
Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu (
Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo
jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko
Okinawa,Japan.
Tunatumaini kwamba chama cha "JUNDOKAN SO HONBU" kitapata
usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei
Rumadha Fundi mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Afrika mashariki na
Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama
hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza.
Alimalizia hivyo; Sensei Rumadha
No comments: