LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAKIKA NDOA NI BARAKA TELE. TAZAMA TAMATI YA USIKU WA MISS JANE JULIUS WA JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Usiku wa kuamkia leo, Julai 30,2016 ilikuwa siku ya kumuaga (Sendoff) Miss Jane Julius mkazi wa Ghana Jijini Mwanza ambae anatarajiwa kuoelewa na Bwana Manase John mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza.

Sendoff ilifanyika katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza na kunogeshwa na Master Of Ceremonies, Katumba Maduwa, akisaidiana na Mc Magoma huku mwimbaji Zarina akitumbuiza vyema katika Sendoff hiyo iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali.

Kulia katika picha ya juu ni bibi harusi mtarajiwa Jane John (kushoto) ambae anatarajiwa kufunga ndoa na Manase John (hayuko pichani), Agost 13,2016 Sengerema, akimtafuta mchumba wake katika Sendoff hiyo, tukio ambalo liliwavutia wengi kutokana na uchangamfu na furaha aliyokuwa nayo bibi harusi huyo mtarajiwa.
Na BMG
Hatimae bibi harusi mtarajiwa akampata mchumba wake, ni full mahagi.
Full maupendo
Maharusi watarajiwa, Manase John (kushoto) na Jane Julius (katikati) wakiingia ukumbini huku mwimbaji Zarina (kushoto) akiimba live na kunogesha sendoff hiyo.
Maharusi watarajiwa, Manase John (kushoto) na Jane Julius (katikati) wakiingia ukumbini
Maharusi wakiingia ukumbini kwa madaha ishara ya upendo
Bibi harusi akionyesha zawadi aliyomuandaliwa mmewe mtarajiwa mbele ya wageni waalikwa ambayo ni saa yenye nembo ya msalaba ishara ya kumcha Mungu katika ndoa yao.
Mama mkwe (mama wa bibi harusi) akionyesha furaha yake ukumbini huku akicheza kwa furaha tele
Maharusi watarajiwa wakati wa msosi...Na iwe hivyo nyakati zote Manase, maana wanandoa ni kusaidiana.
...Nimeamua kuolewa na wewe daddy wangu na sikulazimishwa na mtu, nilijitunza muda mrefu kwa ajili yako, Nakupenda sana...
Bibi harusi mtarajiwa pamoja na marafiki zake wakifungua mziki, kulia ni Mwimbaji Zarina.
Bibi harusi mtarajiwa pamoja na marafiki zake wakifungua mziki, kushoto ni Mwimbaji Zarina.
Kulia ni Zarina, Kushoto ni Mc Magoma na katikati namuona Master Of Ceremonies, Katumba Maduwa, wakinogesha Sendoff ya Jane Julius.
Wageni waalikwa katika ubora wao kwenye kusakata ngoma
Bwana Harusi Mtarajiwa, Manase John (kushoto) akiwa na Mkewe Mtarajiwa, Jane Julius (kulia), wakichumu mbele ya wageni waalikwa kama ishara ya kupendana kwa dhati.
Proudly Sponsored by Mc Katumba, 0786509898 or 0767509898.

No comments:

Powered by Blogger.