LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT WAMLILIA MWANAHABARI MAREHEMU JOSEPH SENGA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita   Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kinaungana na Taasisi nyingine zote, watanzania na Ndugu wa marehemu kwa kifo cha Mwandishi Joseph Senga (pichani).

Chama tunaamini kuwa, Senga alikuwa Mwandishi aliyeipenda kazi yake ndani ya tasnia ya habari, ni vigumu pengo lake kuzibwa mara moja lakini tunaamini mbegu alizoziacha zitachipua na kuzaa matunda mengi kama yeye.

Tunawapongeza wanasiasa na watumishi wote walioweka tofauti zao pembeni na kuungana na Wanahabari kwenye kumlilia mpendwa wetu Senga.

Tunawaomba waandishi wote kujitokeza kwa wingi hasa wale walioko kanda ya Ziwa kujitokeza kwenye mazishi ya mpendwa wetu. Tuna amini sisi tulimpenda lakini mungu.alimpenda zaidi.
Umekwenda shujaa wetu daima tutakukumbuka kupitia vielelezo vya kazi zako.

Edwin Soko
Mwenyekiti
OJADACT

No comments:

Powered by Blogger.