LIVE STREAM ADS

Header Ads

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LAJIPANGA SIKUKUU YA EID EL FITRI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, akiongea na Wanahabari.
Wananchi mkoani Mwanza wakiwemo waumini wa dini ya Kiisalamu, wametakiwa kusherehekea vyema Sikukuu ya Eid El Fitr bila viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmad Msangi, ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na namna jeshi hilo lilivyojipanga kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa sikukuu hiyo.

Amesema jeshi la polisi limejipanga vyema kuwadhibiti wale wote watakaoonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani katika sikukuu hiyo.

"Ni marufuku kuendesha vyombo vya moto huku umelewa, marufuku kuwakusanya watoto kwenye kumbi za muziki bila kuwa na kibali au kuwakusanya watoto kwenye maeneo ya kuogelea". Alisema Kamanda Msangi na kuongeza kwamba atakaekiuka hayo atishia rumande, chumba cha wagonjwa mahututi au hata mochwari hivyo ni vyema wananchi wakawa waangalifu.

Tanzania leo imeungana mataifa mengine duniani kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr inayofanyika baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo ni nguvo ya nne kati ya nguvo tano mhimu kwa waumini wa dini ya kiislamu.

No comments:

Powered by Blogger.