LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMBO YA DODOMA SI MCHEZO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Alphonce Tonny Kapela kutoka Metro Fm Mwanza (kushoto) na George Binagi-GB Pazzo kutoka Lake Fm pia Mwanza na BMG, tukifuahia matunda mjini Dodoma.

Sisi ni baadhi ya Wanahabari tuliotoka mkoani Mwanza, kuhudhuria shughuli za Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma uliofanyika jumamosi Julai 23,2016 na Maadhimisho ya Mashujaa hii yaliyofanyika jana Julai 25,2016, muda wetu wa kukaa Dodoma umefikia tamati leo Julai 26,2016.

Tumebaini kwamba Dodoma ni Mji mzuri ambao miaka michache ijayo, utakua miongoni mwa miji inayovutia zaidi nchini Tanzania. Hii ni kutokana na kupangiliwa vyema katika ujenzi wake.

Pia viongozi wa Serikali wakiwemo Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu Mawaziri pamoja na watendaji wengine, kuhamia mkoani Dodoma, ni fursa nyingine kubwa katika mji huu ambayo itaongeza kasi yake katika ukuaji wake.

Ni wasaa mzuri kwa wakazi wa Dodoma kuanza kuwekeza katika katika uwekezaji wa aina mbalimbali kulingana na uhitaji ikiwemo ujenzi wa hoteli za kisasa. Naamini sasa kupata kiwanja Mjini Dodoma ni lazima utoke jasho. Gharama za viwanja zitapanda maradufu.

Japo ipo changamoto ya kiuzalishaji ikiwemo katika mazao ya chakula mkoani Dodoma, lakini hiyo si sababu ya kuufanya mji huu kupunguza kasi yake ya ukuaji unaoonekana sasa.

Tunawashukuru Dodoma kwa ukarimu wenu japo gharama za maisha ziko juu hususani kwa baadhi ya misimu. 

Tuwatakieni kila la kheri Wana-Idodomya, tutarudi tena Mola akijaalia ili japo tupate kiwanja lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamia mkoani Dodoma, wenu katika kazi, wana-habari-Mwanza.
Alphonce Tonny Kapela kutoka Metro Fm Mwanza (kulia) na Vesterjtz kutoka Afya Radio Mwanza (kushoto).
GB Pazzo (kushoto) na Msolid Pure (kulia), mawasiliano yalianzia whatsupp na hatimae wawili hawa wameweza kukutana live Mjini Dodoma.
Kutoka kushoto ni GB, Solid Pure, Dr.Konny, ndani ya Idodomya
Marafiki kutoka ABM Radio ya Mjini Dodoma
Usafiri wa Bajaji mjini Dodoma unachukua nafasi kubwa pia. Hapa ni mmoja wa madereva wa bajaji mkoani Dodoma ambae asilia yake ni mkoani Mwanza, akishow love na GB (kulia).

No comments:

Powered by Blogger.