LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI ASISITIZA JUU YA KAULI YAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Dkt.John Pombe Magufuli (katikati), akiweka ngao na mkuki katika Maadhimisho ya Siku ya Majushaa ambayo Kitaifa imefanyika leo katika Uwanja wa Mashujaa mkoani Dodoma.

Akitoa salamu zake kwa wananchi wakati wa maadhimisho hayo, Rais Magufuli amewasihi wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa siasa kuhakikisha wanailinda na kuihubiri amani huku akisisitiza kwamba anataka katika maisha yake hata kama atatangulia mbele za haki aiache Tanzania yenye amani.

Pia amerudia kusisitiza juu ya kauli aliyoitoa juzi jumamosi katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi kwamba viongozi wote wa Serikali wakiwemo mawaziri wahakikishe wanatoka Jijini Dar es salaam na kuhamia mkoani Dodoma yalipo Makao Makuu ya Tanzania.

Ambapo kauli hiyo imeungwa mkono na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambae amewataka Mawaziri wote kuamia mkoani Dodoma huku akiongeza kwamba anatarajia kuhamia mkoani Dodoma mwezi wa tisa mwaka huu hivyo Waziri wa Nchi pamoja na Katibu Mkuu wahakikishe ujenzi wa nyumba yake mkoani Dodoma.
Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) kwenye maadhimisho ya Mashujaa mjini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) katika maonyesho hayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Polisi, Ernest Mangu (kulia).
Baadhi ya maofisa wa jeshi wakiwa katika picha ya pamoja
Kumbukumbu zikiendelea ambapo kushoto GB kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza nae alikuwa katika maadhimisho hayo.
Kutoka Afya Radio Mwanza, Vesterjtz (kushoto) nae alikuwepo

No comments:

Powered by Blogger.