LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATENDAJI WA JIJI LA MWANZA WAJIKUTA KATIKA WAKATI MGUMU BAADA YA KUFUNGIWA NJE YA GETI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Picha kutoka maktaba, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza alipokuwa akisisitiza watumishi wa jiji hilo kuchapa kazi ili kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli, katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza ambalo lilifanyika hivi karibuni.

Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwazuia kuingia ofisini.

Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kiburwa Kibamba, amechukua maamuzi hayo mapema hii leo asubuhi, baada ya watumishi hayo kuchelewa kuwasili ofisini jambo ambalo limeonekana kumkera.

BMG imedokezwa kwamba baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza, wamekuwa na desturi ya kuchelewa ofisini jambo ambalo limekuwa likimkera Mkurugenzi huyo mpya.

Baadhi ya watumishi waliokumbana na kadhia ya kufungiwa nje ya geti, hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo ambapo wengi wao wameonekana kupigwa na butwaa kutokana na hatua zilizochukuliwa na Mkurugenzi huyo.

No comments:

Powered by Blogger.