LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA MKOANI MARA AANZA KUPAMBANA NA WATUMISHI WASIO WAADILIFU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na PETER FABIAN, RORYA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya, Charles Chacha, amekuchukua hatua za kupambana na watumishi wanaomzunguka na kutafuna fedha za mapato ya ndani kwa kumsimamisha Mhasibu Msaidizi wa Mapato, Bahati Lwoga, aliyekuwa kitengo cha Mapato kwa kutajwa na Madiwani kuwa yeye ndiye chanzo cha Halmashauri hiyo kukusanya mapato kiduchu .

Hatua hiyo baada ya uongozi wa CCM Wilaya chini ya Mwenyekiti wake, Samweli Kiboye, Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo (CCM), Madiwani na wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu maalumu ya Wilaya kilichokutana kumuomba Mkuu wa Wilaya hiyo, Simon Chacha, kukutana na Mkurugenzi na kufatilia suala la kushuka kwa mapato ya Halmashauri na kukusanya kwa asilimia 30 badala ya asilimia 100.

Jana Mkurugenzi Chacha, alieleza kwamba tayari ameishachukua hatua ikiwemo kumuondoa Bahati Lwoga na kumsimamisha kazi baada ya kuhamishia idara ya Elimu kisha kumpeleka kuhudumu kwenye Kata lakini mtumishi huyo akaenda likizo bila ruhusa ya Mkurugenzina ikiwa ni kinyume na taratibu, kwa sasa tunapitia  taarifa mbalimbali za makusanyo za ofisi ya Mipango na Uhasibu.

“Afisa Mapato naye tunaandaa utaratibu wa kuchunguza na kupitia taarifa zake atakapoziwakilisha kwenye Kamati ya Fedha na Mipango itatoa nini kifanyike juu ya Afisa Mapato Mkuu, Martin Kanyambo wa Halmashauri na kama taarifa zake zitaonyesha kuwepo uzembe tutachukua hatua za kimaadili, lakini tayari nimeisha mwagiza Mwekahazina (Seben Mwalutamwa) kuongea umakini kwa timu ya ukusanyaji mapato,”alisema.

Aidha aliomba muda ili kufatilia ili atakapochukua hatua za kimaadili ikibainika kuwepo njama za makusudi na uzembe wa watumishi katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kutoka katika vyanzo vilivyopo ikiwa ni pamoja na Mialo, Minada ya mifugo na Magulio katika Kata zote 21 zilizo katika Tarafa za Girango, Nyancha, Luoimbo na Soba kwenye msimu wa fedha 2015/2016 ulioishia Juni 2016.

Akijibu malalamiko yaliyotolewa nawaheshimiwa Madiwani kwa Mkuu wa Wilaya hiyo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM juu ya kuwepo vitabu vya stakabadhi visivyo halali na kutumiwa na watendaji kukusanyia mapato, Chacha aliomba kulifanyia kazi kisha kutoa taarifa kwa Madiwani, Mkuu wa Wilaya na viongozi wa CCM kikiwemo hatua zitakazochukuliwa endapo itabainika watumishi kushiriki.

“Tumepewa jukumu la kusimamia watumishi wezetu, kusimamia mapato na miradi ya maendeleo katika sekta zote znazotoa huduma kwa wananchi ili thamani ya fedha iandane na mradi uliotekelezwa na katika kiwango kinachokubalika na BQ ni agizo la Rais Dk John Magufuli aliyetuteuwa na kula kiapo cha maadili ya utumishi wa umma hiyo nimejipanga kuyasimamia hayo kwa nguvu na umakini,”alisema.

Chacha, alisema kwamba kutokana serikali kubadilisha  utaratibu wa makusanyo ya mapato ambapo ukusanyaji utakuwa chini ya Halmashauri kwa asilimia 100 si Mawakala kama ulivyokuwa huko nyuma wamejipanga kutumia watumishi, watendaji wa Kata na Vijiji kwa kushirikiana na Madiwani katika Kata zote 21 ili kufikia lengo la makusanyo ya  mwaka 2016/2017, Rorya inataraji kukusanya Sh bilioni 1.4 mapato ya ndani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha, ametoa wito kwa wataalam na watumishi wa Halmashauri hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viapo vya maadili ya utumishi wa umma na taaluma zao badala yakujitumbukiza katika wizi na mbinu chafu za kutafuna fedha za serikali pamoja ikiwemo kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo  jambo ambalo serikali ya awamu ya tano halitavumilia zaidi ya wahusika kuwawajibisha.

No comments:

Powered by Blogger.