LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAHABARI JIJINI MWANZA WAMLILIA MAREHEMU MWALIMU SOKORO, ALIEKUWA WA VIPINDI BARMEDAS TV.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Aliekuwa Mkuu wa Vipindi kwa miaka mingi katika kituo cha runinga cha Barmedas Tv cha Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki dunia jumamosi julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Kifo chake kimesababisha majonzi makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo waandishi wa habari Jijini Mwanza ambao baadhi yao walipitia mikono ya Sokoro aliefahamika kwa jina maarufu la Mwalimu kutokana na ujuzi wake katika kufundisha nyimbo za Injili hususani kucheza na kinanda pamoja na ubobeaji wake katika taaluma ya habari.

Enzi za uhai wake alikuwa Mwalimu wa kwanza wa Kwaya ya AICT Makongoro waliowahi kutamba na wimbo wa Kekundu huku pia akiwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza katika kituo cha runinga cha Barmedas Tv Cable ambacho awali kilikuwa kikipatikana kwa njia ya cable tu kabla ya hivi karibuni kupatikana katika ving'amuzi mbalimbali.

Mwalimu Charles Sokoro alizaliwa mwaka 1965 na mauti yamemfika mwaka huu 2016 akiwa na miaka 51. Ratiba ya Mazishi ni kama ifuatavyo;
1.Siku ya Jumatatu (18/7/2016 )  saa 10:00 jioni, Mwili wa Marehemu kuwasili kutoka hospitalini Bugando kuelekea Kanisa La AICT Makongoro

2.Siku ya Jumanne (19/7/2016) Kanisa La AICT Makongororo
~Saa 6:00 mchana IBADA ya Kumuaga Mareemu

~Saa 7:30 mchana Safari ya kuelekea Malaloni (Makaburini Kitangiri)
~Saa 8:30 Chakula na baadaye kuhitimisho.
Wanahabari Jijini Mwanza wakieleza namna walivyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake
Wanahabari Mwanza wakieleza namna wavyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake.

Ni juzi tu Tasnia ya Habari ilipata pigo kwa kumpoteza Mwandishi mbobezi kwenye dimba la michenzo Dada yetu mpendwa Elizabert, na leo (julai 16,2016) tasnia hiyo hiyo imekubwa na msiba mwingine wa kaka yetu Charles Sokoro. HAKIKA msiba wa ndugu yetu Sokoro umetuacha midomo wazi tunahisi kama ni ndoto ya usiku lakini ndio ukweli.

Nani asiye mjua sokoro kwa ukarimu wake kwa kila mtu ? Kiukweli  alikuwa mcheshi asiye na makuu. Aliipenda taaluma yake kwa dhati na kila penye kusanyiko la wanahabari naye alimuwepo.

Hakuonyesha umahiri pekee kwenye tasnia ya habari bali hata kwenye mambo mengine. Nani asiyejua uwezo wake kwenye kupiga kinanda? Nani asiyejua umahiri wake kwenye kuenzi utamaduni wa kiafrika?.

Kipindi chake cha ngoma asilia pale Barmedas Tv kilileta uhalisia wa utamaduni wetu. Sokoro; waandishi wenzako tunakulilia umetuacha kwenye wakati mgumu.

Tutakukumbuka daima, tulikupoenda lakini Mungu kakupenda zaidi na alikuita na umeitika leo haupo nasi. Huu ni wakati mgumu sana kwa tasnia ya habari. Mungu tupe nguvu tumpumzishe mwenzetu kwa mikono yetu miwili.
AMINA!
NAEDWIN SOKO;
MRATIBU, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA (MPC).

No comments:

Powered by Blogger.